• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU YA WATU WAZIMA YAFANYIKA KATA YA MERYA

Posted on: September 20th, 2024

Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima ngazi ya Wilaya yamefanyika leo, tarehe 20 Septemba 2024, katika viwanja vya Shule ya Sekondari Merya, iliyopo Kata ya Merya, Halmashauri ya Wilaya ya Singida yakiongozwa na kauli mbiu “Ujumuishi katika elimu bila ukomo kwa ujuzi, kwa ustawi, amani na maendeleo”. Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wananchi, na washiriki wa programu za elimu ya watu wazima, huku mgeni rasmi akiwa ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Mhe. Elia Digha.

Maadhimisho hayo yamejumuisha burudani na maonesho ya vipaji, ambapo wanafunzi walionyesha umahiri wao kwa kucheza na kuimba mashairi, wakisisitiza umuhimu wa elimu katika kuboresha maisha.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Afisa Elimu ya Watu wazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi Bw. Juma Sabigoro, ameeleza umuhimu wa elimu ya watu wazima katika jamii ambapo inasaidia kuwezesha watu kupata ujuzi juu ya matatizo mbali mbali ili waweze kupambana na mazingira yanayo wakabili katika maisha yao.

“Elimu ya watu wazima ni tendo la kupata na kutumia ujuzi, maarifa na mwelekeo inayoweza kukuwezesha wewe kuishi katika jamii. Inakuwezesha wewe kujitambua na kuweza kukabiliana na mazingira unayo yaishi kwa namna yoyote, kwa hiyo elimu hii inakwenda na mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Tunaposema ni chombo cha ukombozi, ni chombo ambacho hutusaidia katika kutatua matatizo mbali mbali ili tuweze kupambana na mazingira yetu vizuri ipasavyo.” Alisema Bw. Sabigoro

Naye mgeni rasmi Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Elia Digha, aliwapongeza washiriki kwa juhudi zao na kusisitiza umuhimu wa elimu kama nyenzo ya kuondokana na umasikini na kuboresha maisha ya jamii. Pia alihimiza wananchi kutumia fursa zilizopo za elimu bila kujali umri, kwa kuwa kujifunza ni hatua muhimu katika kujiletea maendeleo.

“Dunia hii huwezi kuishi vizuri, huwezi kulala vizuri, huwezi kufanya jambo lolote kama elimu huna. Elimu inamkomboa mtu katika jambo lolote hivyo wazazi hakikisheni watoto wanasoma na nyie wenyewe msome.” Alisema Mhe. Digha

Aidha, vikundi mbalimbali vilivyonufaika na elimu ya watu wazima vilishiriki katika hafla hiyo na kutoa ushuhuda wa jinsi elimu hiyo ilivyo wasaidia kuboresha hali zao za kiuchumi, kupanua ujuzi wao, na kujiongezea kipato huku wakitoa wito kwa wananchi wengine kujiunga na programu za elimu ya watu wazima.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 17, 2025
  • MAENEO YA UWEKEZAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA January 03, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI ZA MUDA July 17, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA PESA ZA MIRADI YA MAENDELEO SEPT 2023 October 18, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA SINGIDA WAPATA MAFUNZO KUHUSU USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KATIKA UWEKEZAJI

    April 03, 2025
  • TAWA YATOA ELIMU YA MBINU ZA KUKABILIANA NA WANYAMA PORI

    April 03, 2025
  • HALMASHAURI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI WATEMBELEA HALMASHAURI YA SINGIDA

    March 28, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AWAASA WALIMU KUEPUKA MIKOPO UMINZA

    March 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.