• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

MHE. GODWIN GONDWE ASIKILIZA MGOGORO WA MIPAKA KATI YA VIJIJI VYA MUNKHOLA NA MSIKII

Posted on: January 10th, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe. Godwin Gondwe, amefanya ziara katika hifadhi ya msitu wa kijiji cha Munkhola kwa lengo la kusikiliza mgogoro wa mipaka kati ya kijiji cha Munkhola kilichopo Kata ya Mgori na kijiji cha Msikii kilichopo Kata ya Munghamo na kushughulikia suala la uvamizi wa hifadhi ya msitu wa kijiji cha Munkhola.

Ziara hiyo ilihusisha wataamu mbali mbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Singida Manispaa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)

Akizungumza katika ziara hiyo, Mhe. Gondwe ameeleza kuwa migogoro ya mipaka na uvamizi wa maeneo ya hifadhi ni changamoto zinazozorotesha maendeleo ya jamii na kuhatarisha uhifadhi wa mazingira. Amewataka viongozi wa vijiji vyote viwili kushirikiana kwa maelewano ili kufanikisha suluhisho la kudumu.

Katika jitihada za kumaliza mgogoro huo, Mhe. Gondwe alitoa maazimio mbalimbali ya utekelezaji, ikiwemo kuwataka wataalamu wa ardhi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Singida kwenda katika eneo hilo ili kuonyesha mipaka rasmi kati ya vijiji hivyo. Aidha, alitoa agizo la kuhamishwa kwa wananchi waliojenda ndani ya hifadhi ya msitu huo ili kuendelea kulinda eneo hilo dhidi ya uharibifu. Pia, alisisitiza kupiga marufuku shughuli zote za kilimo ndani ya hifadhi hiyo, akibainisha kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wale watakaokiuka maagizo hayo.

Mhe. Gondwe alitoa wito kwa wananchi wa vijiji vyote kushirikiana na serikali katika kuhifadhi mazingira na kuhakikisha hifadhi ya msitu wa Munkhola inalindwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 17, 2025
  • MAENEO YA UWEKEZAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA January 03, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI ZA MUDA July 17, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA PESA ZA MIRADI YA MAENDELEO SEPT 2023 October 18, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA SINGIDA WAPATA MAFUNZO KUHUSU USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KATIKA UWEKEZAJI

    April 03, 2025
  • TAWA YATOA ELIMU YA MBINU ZA KUKABILIANA NA WANYAMA PORI

    April 03, 2025
  • HALMASHAURI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI WATEMBELEA HALMASHAURI YA SINGIDA

    March 28, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AWAASA WALIMU KUEPUKA MIKOPO UMINZA

    March 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.