• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

MKUTANO WA WADAU WA UMEME WILAYA YA SINGIDA

Posted on: September 6th, 2024

Maofisa wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Singida,wamefanya mkutano na wadau wa umeme katika wilaya ya Singida. Mkutano huo uliofanyika leo 6/9/2024, katika ofisi za chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Singida,umehusisha madiwani wa wilaya ya Singida wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya, Mhe. Eliya Digha na watendaji wa halmashauri wakiongozwa na mkurugenzi Mhe. Esther Chaula pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Singida,huku lengo la mkutano huo likiwa kutoa elimu kwa wananchi kupitia viongozi wao  juu ya matumizi salama ya miundo mbinu ya umeme,utoaji wa huduma ya umeme kwa wananchi na usimamizi wa miradi ya umeme wilayani humo.

Akizungumza katika mkutano huo,Afisa Uhusiano na Uuduma kwa Wateja (TANESCO) mkoa wa Singida,Bi Rehema Mwaipopo amesema,viongozi wawahimize wananchi kutunza miundombinu ya umeme hasa katika kipindi hiki cha kusafisha mashamba,ambapo nguzo za umeme zilizopita mashambani huchomwa moto hivyo kupelekea kukosekana kwa huduma ya umeme katika wilaya nzima.

“Changamoto nyingine tuliyonayo ni uchomwaji moto wa miundombinu ya umeme  na imekuwa ni kilio kikubwa kwetu.Miezi hii huwa ni miezi ya kusafisha mashamba na nguzo za umeme zimepita kwenye mashamba hayo ambapo wananchi huchoma taka kwenye nguzo.Hivyo tunawaomba viongozi mtusaidie kuwaambia wananchi wasichome moto nguzo za umeme.’’ Alisema Bi Rehema.

Hata hivyo Kaimu Meneja wa TANESCO mkoa wa Singida, Mhandisi Nyerere Ernest amesisitiza juu ya matumizi salama ya umeme ili kuepukana na ajali za umeme katika makazi na maeneo ya kufanyia kazi.

“Nyaya tunazotumia majumbani hatuzipitishi kwenye mabomba maalumu, ila tunazipitisha hivyo hivyo kwenye mapaa ya nyumba.Nyaya zilizopita kwenye mabomba ni salama zaidi, lakini watu kwa kuogopa gharama wanafunga  nyaya bila mabomba, hivyo tusaidine kuwaelimisha watumiaji  wetu wa umeme ili kuzuia ajali, vifo, ulemavu, maumivu, madhara katika familia na marafiki.”Alisema Mhandisi Nyerere.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Singida ameipongeza serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Raisi Dk Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka umeme katika vijiji vyote 84 vya halmashauri ya wilaya ya Singida na kusisitiza kuwa ni wakati wa vitongoji navyo kupatiwa umeme.Vilevile amelipongeza shirika kwa uboreshaji wa utendaji kazi ndani ya shirika.

“Ilikuwa watu wakihitaji kuingiza umeme, sisi kama viongozi kila mtu anakuja kukuuliza kama una mtu TANESCO umsaidie aingize umeme kwenye nyumba yake, lakini kipindi kirefu sasa sijapata mtu anayeniambia nahangaika kuingiza umeme nisaidie,  nisaidie…..kama unamtu TANESCO aniingizie umeme hivyo, maana yake shirika linafanya kazi vizuri.” Alisema Mhe. Chaula.

Aidha Mwenyekiti wa  Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Mhe. Eliya Digha, amesisitiza juu utolewaji wa elimu ya upatikanaji wa huduma ya umeme kwa wananchi. Ametoa rai kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kufika kwa wananchi kuwaelimisha juu ya uingizaji wa umeme kwenye makazi yao.

“Mtu ana nguzo mita thelathini au chini ya mita thelethini,lakini bado anasema mimi sijawekewa umeme wapeni wananchi  hiyo elimu ili umeme uenee kwa kasi kubwa.”Alisema Mheshimiwa Digha.

Hata hivyo waheshimiwa madiwani walipata nafasi ya kufikisha kero za wananchi wao kwa njia ya maswali na maoni kwa  maofisa wa  Tanesco kuhusiana na huduma ya umeme, ambapo maofisa  waliahidi kwenda kuyafanyia kazi maoni hayo.

Matangazo

  • TANGAZO LA BVR May 11, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 17, 2025
  • MAENEO YA UWEKEZAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA January 03, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI ZA MUDA July 17, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA SINGIDA WAPATA MAFUNZO KUHUSU USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KATIKA UWEKEZAJI

    April 03, 2025
  • TAWA YATOA ELIMU YA MBINU ZA KUKABILIANA NA WANYAMA PORI

    April 03, 2025
  • HALMASHAURI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI WATEMBELEA HALMASHAURI YA SINGIDA

    March 28, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AWAASA WALIMU KUEPUKA MIKOPO UMINZA

    March 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.