• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

MKUU WA MKOA WA SINGIDA, MHE. HALIMA DENDEGO AZINDUA BONANZA LA UCHAGUZI MTINKO

Posted on: September 21st, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, alizindua rasmi Bonanza la Uchaguzi lililofanyika tarehe 21 Septemba 2024, katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Kata ya Mtinko, kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Malolo. Bonanza hili, lililoandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa, lililenga kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Bonanza hilo,lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, viongozi wa kisiasa, watumishi wa umma, na wananchi kwa ujumla na kuhusisha michezo mbalimbali kama mpira wa miguu, mbio za mita 100, kuvuta kamba, mashindano ya chakula, mbio za magunia, na kufukuza kuku.

Akitoa elimu ya uchaguzi, Mratibu wa uchaguzi Mkoa wa Singida, Hussein Mwatawala aliwaelimisha wananchi kuhusu sifa za mpiga kura na zoezi la uandikishaji na uboreshaji wa daftari la kudumu la kupiga kura.Alieleza kuwa uandikishaji mpya utafanyika kuanzia tarehe 25 Septemba hadi 1 Oktoba, ambapo vijana waliofikisha miaka 18 wataandikishwa na wakazi wapya wa eneo husika wataboresha taarifa zao.

“Kwenye suala la kujiandikisha zipo baadhi ya sifa zilizoainishwa lakini sifa kubwa ni hii ya miaka kumi na nane lakini tuhakikishe wanaoandikishwa ni wakazi wa eneo husika.Hivyo basi kuanzia tarehe 25 mwezi huu mpaka tarehe 1 octoba kutakuwa na uboreshaji wa daftari la wapigakura,na tukisema uboreshaji tunamaana zifuatazo;moja,kuna wale wananchi waliofikisha umri wa miaka kumi na nane wataandikiashwa kwenye daftari la kudumu la kupiga kura,lakini kuna watu ambao walikuwa maeneo mengine lakini mfano wamekuja kuhamia wanaweza kuwa ni wafanyakazi au vinginevyo,hivyo wao watatakiwa kuboresha taarifa zao kwa kwenda kituoni.” Alisema Mwatawala

Katika bonanza hilo, huduma za afya pia zilitolewa, ikiwemo vipimo vya virusi vya ukimwi, kifua kikuu, shinikizo la damu, na uchangiaji damu. Dkt. Shaban Mahenge kutoka Hospitali ya Wilaya ya Singida aliwahamasisha wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Mpox (homa ya nyani), huku akiweka msisitizo juu ya maambukizi kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kupitia kula nyama pori na kugusana kwa majimaji ya mwili.

“Ugonjwa huu unatokana na maambukizi kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.Ugonjwa huu kwasababu unapatikana kwenye mapori,hata wanyama wengine sasa wamekuwa na virusi hivi,na vinaweza kuhama kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu,kutokana na binadamu kula nyama pori.Ugonjwa huu una dalili,kama zilivyo dalili kama homa,maumivu ya mgongo,kuumwa na kichwa pamoja na vidonda vya koo.Namna ya kujikinga na ugonjwa huu ni kuchukua tahadhari,kwani muingiliano wa majimaji yaliyoko mwilini kama mate, makamasi, jasho na damu yanaweza kusababisha ugonjwa huu.Vilevile ugonjwa huu unaweza kusababishwa kwa kujamiiana pasipo kutumia kinga”. Alisema Dkt. Mahenge.

Akimuwakilisha mgeni rasmi katika kutoa hotuba, Katibu Tawala za Mikoa, Mkoa wa Singida,Dkt. Fatuma Mganga,amewaasa makatibu kata kutoa elimu ya uchaguzi kwa wananchi kwa kupitia mabonanza kama haya katika kata zao ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.

“Kwa niaba ya Mheshimiwa Mkuu wa mkoa mimi niwaelekeze watendaji wa kata na waheshimiwa madiwani twendeni tukatengeneze mabonanza ya kata ili watu wengi waweze kupata hii elimu.Kwa kasi hii hatuwezi kufika lakini kwenye kata zipo shule,zipo timu mbalimbali,akina Mama na akina Baba watavuta kamba kule, watakimbiza kuku kule na kwakufanya hivyo tukiwa na mabonanza ya uchaguzi kwa kila kata ninaamini tutawafikia wanasingida wengi na elimu itafikia watu wengi.” Alisema Dkt. Fatuma Mganga.

Pia Dkt. Maganga aliikazia maelezo ya mratibu wa uchaguzi wa mkoa,kwa kusema kuwa kila mtu anatakiwa kujiandikisha upya kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa, hata kama walijiandikisha katika chaguzi za nyuma, kwani orodha ya wapiga kura inaboreshwa kila mwaka. Alisisitiza umuhimu wa kujitokeza kwa wingi ili kuhakikisha ushiriki wa wananchi unakuwa mkubwa.

Matangazo

  • TANGAZO LA BVR May 11, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 17, 2025
  • MAENEO YA UWEKEZAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA January 03, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI ZA MUDA July 17, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA SINGIDA WAPATA MAFUNZO KUHUSU USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KATIKA UWEKEZAJI

    April 03, 2025
  • TAWA YATOA ELIMU YA MBINU ZA KUKABILIANA NA WANYAMA PORI

    April 03, 2025
  • HALMASHAURI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI WATEMBELEA HALMASHAURI YA SINGIDA

    March 28, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AWAASA WALIMU KUEPUKA MIKOPO UMINZA

    March 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.