• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

MKUU WA WILAYA YA SINGIDA KATIKA KIKAO KAZI CHA LISHE NA WATAALAMU WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA

Posted on: February 14th, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Mhandisi Paskasi Muragili akizungumza na Maafisa Lishe, Wakuu wa Idara  na Watendaji wa Kata katika kikao kazi cha Lishe kilichofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Muragili amewaagiza Maafisa Lishe wakishirikiana na Watendaji wa Kata na viijiji kuhakikisha elimu ya Lishe bora inawafikia wananchi wote, kwani lishe bora hujenga afya bora na kwa kuzingatia ulaji bora jamii itaepukana na changamoto za udumavu wa akili kwa watoto na hivyo kuleta tija katika ufaulu wa wanafunzi mashuleni.

Akitolea taarifa juu ya hali ya lishe mashuleni, mwalimu Juma Sabigoro (wa tatu toka meza kuu) kwa niaba ya  Afisa Elimu Wilaya ameelezea kuwa kakribani shule zote za Halmashauri ya Wilaya ya Singida zinapata Lishe kwa kuanzia na kifungua kinywa cha uji. Mwalimu Sabigoro ameongezea kwa kusema hata hivyo jitihada zinaendelea kufanywa na bodi za shule kuendelea kuhimiza wazazi wa wanafunzi umuhimu wa kuchangia chakula mashuleni ili watoto wao waweze kupata lishe bora na hivyo kuchangia ufaulu wa mwanafunzi huyo. Mwalimu huyo ameongezea na kusema kuwa takribani shule zote zenye maeneo ya kilimo wamehakikisha yamelimwa ili kuongezea uwezo wa shule kulisha wanafunzi wake na hivyo kuwa na afya bora.

Akitoa taarifa jumuishi ya lishe Mratibu wa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Bi: Neema Swai ameelezea kuwa kwa kipindi cha robo ya kwanza na robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/ 2023 huduma ya Lishe kwa mama mjamzito na mtoto imeendelea kuboreshwa katika vituo vya afya 40 vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida ambapo idadi ya wakina mama wanaojifungulia majumbani imepungua kutoka wakina mama193 hadi  wakina mama 89. Huduma za utoaji wa chanjo ya mama na mtoto pamoja na kinga ya malaria dhidi ya mama mjamzito imeendelea kutolewa kwa kushirikiana na Watoa Huduma Ngazi ya Jamii. Wataalamu wa afya wameendelea kutoa elimu juu ya matumizi ya chumvi yenye madini joto kwani ina mchango mkubwa katika lishe bora, hata hivyo asilimia 57.3 ya chumvi inayotumika katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida ina madini joto. Afisa Lishe huyo ameongezea kusema kuwa jitihada jumuishi zinahitajika katika kuendelea kutoa elimu katika jamii juu ya umuhimu wa mzazi kujifungua katika kituo cha afya  ili kutokomeza kabisa vifo vya mama na mtoto.   

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Mhandisi Paskasi Muragili ametoa onyo kuwa ni marufuku kwa mama mjamzito kujifungulia nyumbani na endapo taarifa itatolewa ya mzazi aliyejifungua nyumbani maelezo ya kina waweze kutolewa na Mtaalamu wa Afya kuwa ni mazingira gani yaliyopelekea tukio hilo.  Akiongea na Watendaji wa Kata, Vijiji na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Mkuu huyo wa Wilaya amekemea vikali tabia za baadhi ya walimu mashuleni kuuza au kutumia chakula cha shule, au mazao yatokanayo na shamba la shule kwa maslahi yao binafsi.   

Mhe. Muragili ameendelea kusisitiza Maafisa Lishe na Watendaji wakishirikiana na Watoa Huduma Ngazi ya Jamii kuendelea kutoa elimu katika jamii juu ya umuhimu wa Lishe bora, pia matumizi ya chumvi yenye madini joto na kuagiza Wataalamu wa Lishe kupiga marufuku na kukamata chumvi zinazoingizwa sokoni zisizo na madini joto kwani ukosefu wa madini joto katika mwili wa binadamu una madhara katika afya ya jamii.


Matangazo

  • TANGAZO LA MARUDIO NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA July 02, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA UFADHILI WA MAFUNZO YA KUJENGEWA UWEZO KWA WATUMISHI WA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI July 02, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA KUHU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE NGAZI YA MKOA NA WILAYA KWA MWAKA 2025 June 10, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • ZIARA YA DC GODWIN GONDWE, KUKAGUA MAANDALIZI YA UJIO WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, SINGIDA DC.

    June 21, 2025
  • WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO WA USIMAMIZI WA UTENDAJI KAZI KATIKA UTUMISHI WA UMMA (PEPMIS)

    June 20, 2025
  • TASWIRA YA DARAJA LA JP MAGUFULI, (KIGONGO - BUSISI)

    June 19, 2025
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA DARAJA LA JP MAGUFULI (KIGONGO - BUSISI)

    June 19, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.