• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida ashiriki Ibada ya Mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mrama

Posted on: September 4th, 2024


Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, ukiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Elia Digha, umeungana na waombolezaji katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mrama, Mhe. Charles Abeid Msonia. Ibada hiyo imefanyika nyumbani kwa marehemu kata ya Mrama, tarehe 04/09/2024, na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, wawakilishi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, wananchi wa Kata ya Mrama na maeneo jirani.

Akizungumza katika ibada hiyo, Mhe. Digha alimsifu marehemu kwa utendaji wake bora kama kiongozi wa Halmashauri.

“Marehemu Mhe. Msonia amehudumu katika Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Singida kwa miaka tisa. Alikuwa diwani mwaminifu, mchapakazi na mtetezi wa wananchi wa Kata ya Mrama. Hakuwa na makuu, alikuwa mcheshi, na alipenda sana muziki. Kifo chake kimetuachia pengo kubwa ambalo ni vigumu kuliziba." alisema Mhe. Digha.

Naye Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Mhe. Ramadhani Abeid Ighondo, alitoa salamu zake za rambirambi. Alimshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri kwa ushirikiano alioutoa wakati wa ugonjwa wa Mhe. Msonia.

"Tangu Mhe. Msonia alipoanza kuumwa, ulikuwa naye karibu, na umejaribu kutoa msaada wa kila namna. Napenda kuwahakikishia wananchi wa Kata ya Mrama kuwa masuala yote mliyokuwa mkimfikishia marehemu, yataendelea kufanyiwa kazi. Pia, tuheshimu utaratibu wa serikali, ambapo mtendaji wa kata ataendelea kukusanya kero zenu." alisema Mhe. Ighondo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mhe. Martha Mlata, alikumbusha mchango wa marehemu katika maendeleo ya kata hiyo, akieleza jinsi Mhe. Msonia alivyojitahidi kuunganisha Kata ya Mrama na serikali kuu chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dr. Samia Suluhu Hassan. "Amefanikisha kuletwa kwa maendeleo makubwa katika kata hii, na hilo ni jambo ambalo hatutakaa tusahau" alisema. Pia Mhe. Mlata alimteua Mhe. Aysha Rose Matembe kuwa Diwani wa kata ya Mrama mpaka hapo serikali itakavyoamua vinginevyo.

Mhe. Charles Abeid Msonia alizaliwa mwaka 1962 katika Kijiji cha Mwakiti, Kata ya Mrama, Wilaya ya Singida. Alisoma Shule ya Msingi Sekoutoure na kuhitimu mwaka 1981. Mhe. Msonia alibatizwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) Kijota mwaka 1993 na baadaye kufunga ndoa na mkewe Bi. Elizabeth S. Idabu mwaka 1999. Ameacha mjane na watoto watano, wanne wa kiume na mmoja wa kike, pamoja na wajukuu wanne.

Kipindi cha uhai wake Mhe. Msonia alijishughulisha na kilimo, ufugaji, na biashara pia aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kanisa. Alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Kata ya Mrama kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, na Diwani wa Kata hiyo tangu mwaka 2015 hadi umauti ulipomkuta.

Matangazo

  • TANGAZO LA BVR May 11, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 17, 2025
  • MAENEO YA UWEKEZAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA January 03, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI ZA MUDA July 17, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA SINGIDA WAPATA MAFUNZO KUHUSU USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KATIKA UWEKEZAJI

    April 03, 2025
  • TAWA YATOA ELIMU YA MBINU ZA KUKABILIANA NA WANYAMA PORI

    April 03, 2025
  • HALMASHAURI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI WATEMBELEA HALMASHAURI YA SINGIDA

    March 28, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AWAASA WALIMU KUEPUKA MIKOPO UMINZA

    March 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.