• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

NAIBU KATIBU MKUU MWAMBENE AHIMIZA USHIRIKIANO SEKTA YA ELIMU

Posted on: January 29th, 2025

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu, Atupele Mwambene amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa (Elimu) Wakuu wa Divisheni za Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuwa na ufanisi mzuri utakaosaidia kutimiza malengo ya serikali kwenye sekta ya elimu.

Mwambene ameyasema hayo leo Januari 27, 2025 wakati akifungua kikao Kazi cha Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Elimu katika kipindi cha Julai hadi Desemba, 2024 kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa (Elimu) Wakuu wa idara za Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari kilichofanyika Mkoani Msingida.

Amesema watumie kikao hiko kutafakari kwa kina, kujengeana uzoefu, kubadilishana mbinu na kushirikishana katika masuala mbalimbali yanayohusu utendaji kazi na utekelezaji wa maelekezo na shughuli zote za serikali za sekta hiyo ili kuimarisha utekelezaji. Mwambene amesema kuwa serikali imefanya jitihada kubwa katika kuimarisha sekta ya elimu hususani katika shule za msingi na sekondari nchini na kuleta mafanikio mbalimbali ikiwamo kuongezeka kwa udahili wa wanafunzi katika ngazi mbalimbali ikiwemo sekondari kufikia 3,087,870 mwaka 2024 na shule za msingi kufikia 11,391,185 mwaka 2024.

Aidha, amewapongeza viongozi hao kwa kusimamia vigezo walivyowekeana vya kupimana na utendaji kazi ambavyo vimeongeza ufaulu katika mitihani ya kitaifa kwa Darasa la Nne kutoka asilimia 83.3 2023 hadi asilimia 86 mwaka 2024, Darasa la Saba kutoka asilimia 80.58 hadi asilimia 80.87 mwaka 2024.

“Kidato cha Pili kutoka asilimia 85.31 hadi asilimia 85.41 mwaka 2024, na Kidato cha Nne kutoka asilimia 89.36 mwaka 2023 hadi asilimia 92.37 mwaka mwaka 2024’’ amesema

Naye, Mkurugenzi, Idara ya Usimamizi wa Elimu, Ofisi ya Rais -TAMISEMI Dkt. Emmanuel Shindika amesema lengo la kikao hicho ni kufanya tathmini ya kina ya shughuli za elimu zilizopangwa kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba 2024.

Awali, Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga ametoa wito kwa Maofisa hao kila mmoja katika eneo lake kubuni mbinu na utaratibu wa watoto kupata chakula shuleni

Matangazo

  • TANGAZO LA KUKODISHWA KWA SHAMBA LA MBEGU LA MPAMBAA September 16, 2025
  • TANGAZO LA WATUMISHI KUHUSU WCF September 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI August 30, 2025
  • TANGAZO LA FURSA ZA KUTOA HUDUMA ZA CHAKULA (CATERING) KATIKA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA September 01, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MKUTANO MAALUM WA MAANDALIZI YA MSIMU WA KILIMO, WILAYA YA SINGIDA.

    October 03, 2025
  • TIMU YA UKAGUZI KUTOKA KIKOSI CHA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, YAFANYA UKAGUZI.

    October 02, 2025
  • MHE. GONDWE ATEMBELEA MIRADI YA LISHE KATIKA SHULE 3 ZA SEKONDARI.

    September 29, 2025
  • USAFI WA MAZINGIRA WAFANYIKA, KATA YA MUGHAMO

    September 26, 2025
  • Angalia zote

Video

WATUMISHI WAPYA WAASWA KUWEKA AKIBA
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.