• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

SINGIDA DC YAZINDUA MSIMU WA UPANDAJI MITI

Posted on: January 16th, 2024

“Kupanda miti ni hatua moja… na kuitunza ni hatua nyingine… ninaomba sana sana... kwa sisi viongozi tuliopo hapa kwa hii miti iliyopandwa hapa leo tuitunze, tuiangalie ” hayo yamesemwa na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Naima Chondo ambaye pia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo katika uzinduzi wa wiki ya upandaji miti iliyofanyika Shule ya Sekondari Mkimbii kata ya Kinyeto Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

Akiongea na wananchi, wadau wa misitu, mazingira pamoja na viongozi wa chama na Serikali, Chondo amewataka wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida kutumia msimu huu wa mvua katika kupanda miti na kuitunza katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Aidha uzinduzi wa msimu wa upandaji miti Wilaya ya Singida umeongozwa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wakishirikiana na wadau kutoka shirika la “Tree For The Future”, pamoja na viongozi kutoka Taasisi ya Mwalimu Nyerere Wilaya ya Singida ambapo zaidi ya miti 400 imepandwa katika eneo hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Mhe. Elia Digha ameitaka jamii ya Singida kuwa na mtizamo chanya katika kutunza mazingira kwa kupanda miti, “katika kuhakikisha mazingira yanakuwa bora ni lazima tupande miti”, alisisitiza Digha. Akibainisha faida za miti ni pamoja na upatikanaji wa hewa safi ya Oksijeni, uvunaji wa hewa ya ukaa, miti ya matunda na miti mingine hutumika katika tiba za magonjwa  na utafiti wa kisayansi.

Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la “Tree For The Future” Singida Ndg. Abraham Mrema amesema mojawapo ya shughuli wanazozifanya ni uoteshaji wa vitalu vya miche ya kivuli na matunda, kupanda miti maeneo ya taasisi binafsi na Serikali  pamoja na kilimo cha bustani msitu. Mrema ametaja faida mbalimbali za kilimo cha bustani msitu ni pamoja na kuongeza usalama wa chakula, chanzo cha vyakula aina mbalimbali vyenye lishe kwa kaya 1318 za wakulima kupitia upandaji wa mboga mboga na miti ya matunda. Hata hivyo Mrema amesema kwa mwaka 2024/ 2025 shirika lake lina mpango wa kupanda jumla ya miti 826,255 katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

Aidha mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Naima Chondo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na RAIS Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo ya wananchi katika Wilaya ya Singida katika sekta za elimu, afya, umeme kupitia wakala wa umeme vijijini (REA), maji na barabara.


Matangazo

  • TANGAZO LA BVR May 11, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 17, 2025
  • MAENEO YA UWEKEZAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA January 03, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI ZA MUDA July 17, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA SINGIDA WAPATA MAFUNZO KUHUSU USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KATIKA UWEKEZAJI

    April 03, 2025
  • TAWA YATOA ELIMU YA MBINU ZA KUKABILIANA NA WANYAMA PORI

    April 03, 2025
  • HALMASHAURI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI WATEMBELEA HALMASHAURI YA SINGIDA

    March 28, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AWAASA WALIMU KUEPUKA MIKOPO UMINZA

    March 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.