• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

TARI WATOA MAFUNZO YA KANUNI ZA KILIMO BORA CHA KOROSHO

Posted on: September 10th, 2024

Wakulima wa zao la Korosho wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida pamoja na maafisa ugani wapokea mafunzo kutoka kwa wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) – Naliendele. Mafunzo hayo yametolewa tarehe 08/09/2024 katika shamba la Mustapha Mwangi (mkulima) lilipo kata ya Ilongero yakiwahusisha wakulima 30 pamoja na maafisa ugani 15 wa wilaya.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Gaspar Mgimiloko amabaye ni mtafiti kutoka TARI alisisitiza umuhimu wa matumizi sahihi na salama ya viwatilifu ili kudhibiti visumbufu vya Korosho, lengo likiwa ni kupunguza athari za wadudu na magonjwa yanayoweza kupunguza uzalishaji na tija ya zao hilo.

Pia, mafunzo hayo yaliangazia upuliziaji wa viwatilifu, matumizi ya mavazi kinga, mbegu bora, utunzaji wa shamba, uchanganyaji wa mazao na upogoleaji. Mgimiloko alibainisha kuwa mafunzo haya ni muhimu kwa maafisa ugani, hasa wale waajiriwa wapya, ili kuongeza uelewa wao kuhusu uzalishaji wa korosho, hususan wanatoka maeneo ambayo hayana uzoefu na zao hili.

 “Lengo la kuwajumuisha wakulima na maafisa ugani tunaamini maafisa ugani tayari wana mafunzo waliyo yapata vyuoni lakini kuna maafisa ugani ambao ni waajiriwa wapya yamkini wanatoka sehemu au kanda ambazo hazilimi zao la Korosho kwa hiyo lengo pia ni kuwaongezea wigo wa uelewa juu ya uzalishaji wa zao la Korosho” Alisema Mgimiloko

Kwa upande wake afisa ugani mifugo kata ya Kinyagigi Vaileth Nyamwonyo ameshukuru uwepo wa mafunzo hayo kwa kumwezesha kuwa na ujuzi wa namna  bora ya uzalishaji wa Korosho. Naye afisa ugani kilimo kata ya Mtinko Emmanuel  Ambrose, alieleza kuridhishwa kwake na mafunzo kwa sababu yatasaidia katika kuelimisha wakulima wengine.

Naye Mkulima Emiliana Lisu kutoka kata ya Kinyagigi ameahidi kuyafanyia kazi mafunzo aliyoyapata ikiwa ni pamoja aina na matumizi sahihi ya viwatilifu, namna nzuri ya upandaji Korosho pamoja na ujuzi wa kuhusu udongo unaofaa.

“Mafunzo haya yamenisaidia mimi kama mkulima wa Korosho kufahamu namna bora ya kulima zao hili na pia nimefahamu udongo unaofaa kwa kuotesha Mikorosho na matumizi sahihi ya viwatilifu.” Alisema Emiliana.

Mmiliki wa shamba lililotumika kwa mafunzo Mustapha Mwangi, alieleza nama mafunzo yalivyomsaidia kufahamu thamani ya kilimo cha korosho na kuboresha shamba lake, ambalo hapo awali halikutoa mavuno mazuri.

 “Nimefaidika na mafunzo haya kwa sababu mambo mengi tulikuwa tunasoma kwenye makaratasi na vitabu ila tunashindwa tuyafanyaje ila kupitia ujio wa mafunzo haya nimefahamu nini hasa cha kufanya ili kuboresha shamba langu kwa sababu mikorosho yangu ilikuwa haitoi mavuno mazuri hivyo sijawahi kuvuna na kupata faida yoyote kupitia hii mikorosho.” Alisema Mustapha Mwangi.

Jumla ya ekari 268 hutumiwa na wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida kulima zao la Korosho.


Matangazo

  • TANGAZO LA BVR May 11, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 17, 2025
  • MAENEO YA UWEKEZAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA January 03, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI ZA MUDA July 17, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA SINGIDA WAPATA MAFUNZO KUHUSU USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KATIKA UWEKEZAJI

    April 03, 2025
  • TAWA YATOA ELIMU YA MBINU ZA KUKABILIANA NA WANYAMA PORI

    April 03, 2025
  • HALMASHAURI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI WATEMBELEA HALMASHAURI YA SINGIDA

    March 28, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AWAASA WALIMU KUEPUKA MIKOPO UMINZA

    March 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.