• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

WALIMU SINGIDA WAJENGEWA UWEZO WA UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI WA KIINGEREZA NA KKK KWA KUZINGATIA MTAALA ULIOBORESHWA MWAKA 2023

Posted on: February 13th, 2024

Hayo yamejiri katika mafunzo yanayoendelea kutolewa ukumbi wa kituo cha walimu (TRC) Halmashauri ya Wilaya ya Singida yanayoendeshwa na Ofisi ya Rais- TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana na Programu ya Shule Bora ambapo imeandaa Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA) ambapo  wawezeshaji kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) wanawezesha walimu wanaofundisha darasa la kwanza kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 12 hadi 16 Februari, 2024. Aidha Mratibu wa mafunzo kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania Ndg. Mbezi Benjamin amewataka walimu wanaofundisha madarasa ya awali na darasa la kwanza kuwa wabunifu na mahiri katika kutumia zana za kufundishia na kujifunza zilizopo katika maeneo yao na hasa katika kuwashirikisha wanafunzi.

Benjamin amebainisha endapo walimu watakuwa mahiri katika kuzingatia mbinu bora na shirikishi za ufundishaji na ujifunzaji wa Kiingereza na KKK (Kusoma, Kuandika na Kuhesabu) kwa kuzingatia mtaala ulioboreshwa wa mwaka 2023 utamuwezesha mtoto kujua KKK na kutamka maneno ya kiingereza kwa ufasaha.

Hata hivyo muwezeshaji kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Joyce Mchilo amebainisha baadhi ya mafanikio yatakayoweza kupatikana baada ya mafunzo kwa walimu wanaofundisha madarasa ya awali na la kwanza ni kumuwezesha mwalimu kufanya maandalizi ya ufundishaji na ujifunzaji kulingana na mtaala ulioboreshwa na kutumia mbinu ya CLT (Communicative Language Teaching) na zana stahiki ili kujenga umahiri wa mwanafunzi katika kuzungumza, kusikiliza, kusoma na kuandika lugha ya Kiingereza.

Mafanikio mengine ni pamoja na kumjengea uwezo mwalimu kutumia mbinu na zana stahiki katika kufundisha stadi za KKK na kubuni mbinu mbalimbali za kufundisha darasa jumuishi kwa ufanisi.

Aidha walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida wameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na RAIS Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea mafunzo haya kwani yamewajengea mbinu bora za ujifunzaji na ufundishaji na hivyo kuwaongezea umahiri katika kufundisha darasani.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA BVR May 11, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 17, 2025
  • MAENEO YA UWEKEZAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA January 03, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI ZA MUDA July 17, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA SINGIDA WAPATA MAFUNZO KUHUSU USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KATIKA UWEKEZAJI

    April 03, 2025
  • TAWA YATOA ELIMU YA MBINU ZA KUKABILIANA NA WANYAMA PORI

    April 03, 2025
  • HALMASHAURI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI WATEMBELEA HALMASHAURI YA SINGIDA

    March 28, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AWAASA WALIMU KUEPUKA MIKOPO UMINZA

    March 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.