• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

DC GONDWE AWAPONGEZA, WAFANYABIASHARA, AHAIDI SERIKALI ITAENDELEA KUTOA ELIMU YA MANUNUZI, ULIPAJI KODI

Posted on: February 13th, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe. Godwin Gondwe, amewapongeza wafanyabiashara wa wilaya hiyo kwa juhudi zao katika kuendeleza biashara na kuchangia mafanikio ya mkoa, huku akiwataka wataalam kutoka Serikalini kuendelea kutoa elimu kuhusu mfumo wa manunuzi wa NeST na ulipaji wa kodi.Mhe. Gondwe ametoa pongezi hizo jana Februari 12, 2025 wakati wa ufunguzi wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Singida, ambalo limefanyika katika Ukumbi wa Jalmin Hoteli, Manispaa ya Singida.

Baraza hilo linalojumuisha wafanyabiashara, taasisi za serikali, sekta binafsi, pamoja na wataalam kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Singida na Wilaya ya Singida, lengo lake ni kuboresha mazingira ya biashara na kujenga ushirikiano mzuri kati ya wafanyabiashara na Serikali.

Akiwahutubia washiriki wa Baraza hilo, Mhe. Gondwe alisema kuwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Singida wamekuwa chachu ya mafanikio ya mkoa huo, na kwamba wanastahili kupongezwa kwa juhudi zao katika kuendesha biashara na kushirikiana na Serikali katika ukusanyaji wa mapato. Alisisitiza kuwa wafanyabiashara wamekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa wilaya hiyo na mkoa kwa ujumla.

“Nawapongeza wafanyabiashara wa Wilaya ya Singida kwa namna wanavyofanya kazi nzuri na namna ambavyo wamekuwa wakishirikiana na Serikali katika ukusanyaji wa mapato,” alisema Mhe. Gondwe.

Pamoja na pongezi hizo, Mhe. Gondwe aliongeza kuwa Serikali imekuwa ikifanya juhudi kubwa kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanapata mazingira bora ya kufanya biashara. Alizitaka idara na vitengo husika kutoa elimu ya kutosha kwa wafanyabiashara kuhusu matumizi ya mfumo wa manunuzi wa NeST (National e-Procurement System) na ulipaji wa kodi, ili kuongeza ufanisi katika biashara na michakato ya manunuzi serikalini.

“Tunawaomba wataalam kutoka Serikalini kuendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu mfumo huu wa NeST pamoja na namna ya kulipa kodi, kwani elimu hii itawawezesha wafanyabiashara kufanyakazi zao kwa ufanisi na kwa kuzingatia sheria,” alisisitiza Mhe. Gondwe.


Matangazo

  • TANGAZO LA MAUZO YA MAZAO YA MISITU December 05, 2025
  • TANGAZO LA BIMA December 05, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI November 20, 2025
  • TANGAZO LA FURSA ZA KUTOA HUDUMA ZA CHAKULA (CATERING) KATIKA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA September 01, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MKUU WA MKOA AMKABIDHI MKURUGENZI MTENDAJI MASHINE YA KULIMIA(POWER TILLER)

    December 01, 2025
  • ZIARA YA KATIBU TAWALA WA MKOA WA SINGIDA, KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO YA HALMASHAURI

    November 27, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA IMEFANYA KIKAO CHA MAFUNZO KWA WATUMISHI WAKE WOTE

    October 26, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA YAADHIMISHA SIKU YA LISHE KITAIFA MWAHANGO

    November 21, 2025
  • Angalia zote

Video

WATUMISHI WAPYA WAASWA KUWEKA AKIBA
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.