Ujenzi wa Miundombinu, Halmashauri ilipokea jumla ya Tsh.1, 879,300,000.00 (Tsh. 1,479,300,000 P4R, Tsh. 300,000,000 Serikali kuu na Tsh. 100,000,000 TEA) kupitia fedhahizi, kazi zifuatazo zimefanyika ukarabati wa maabara 2, ujenzi wa vyumba vya Madarasa 19, ujenzi wa mabweni 10, ujenzi wa matundu ya vyoo 43, ujenzi wa mabwalo 2, makataba 1, ujenzi wa nyumba 4 za walimu na ukamilishaji wa maboma ya vyumba vya madarasa 24 na kuwezesha kuwa na mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia.
Udahili wa kidato cha I umeongezeka kutoka wanafunzi 2,324 kwa mwaka 2015 hadi kufikia wanafunzi 4,314 kwa mwaka 2020 sawa na ongezeko la 54%
Kwa kidato cha V udahili umeongezeka kutoka wanafunzi 147 kwa mwaka 2015 hadi kufikia wanafunzi 429 kwa mwaka 2020.
Vilevile Halmashauri ilipokea jumla ya Tsh.2,443,462,539.73 ikiwa ni fedha za ruzuku ya uendeshaji (Capitation) fidia ya ada (kwa ajili ya ununuzi wa Vifaa, Ukarabati, Mitihani, Michezo, Utawala posho ya madaraka kwa wakuu wa shule kwa Sekondari.
Aidha idadi za Sekondari za ‘A’level zimeongezeka kutoka Shule 2 za Sekondarikwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia Sekondari 4 kwa mwaka 2019/2020.
Halmashauri ya Wilaya ya Singida imendelea kuweka msukumo katika masomo ya Sayansi kwa kuimarisha ufundishaji wa masomo hayo kwa ufanisi kwa kutumia nadharia na vitendo ili kuwavutia wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi. Na hatimaye kupata watalaam wanaohitajika katika sekta mbalimbali. Katika kuweka msukumo huu Halmashauri imekamilisha vyumba vya maabara 17na vyumba 61 vipo hatua ya mwisho ya ukamilishaji, aidha jumla ya shule 11 kati ya 29 zinafanya mtihani wa vitendo kwa masomo yote na shule 18 zimesajili masomo kwa njia ya vitendo pungufu na masomo mawili.