IDARA YA MAENDELEO YA JAMII
Halmashauri imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kutoa mikopo kwa Vijana na Wanawake kwa mujibu wa Ibara za 60 na 61 zinazoitaka Halmashauri kutenga fedha na kuviwezesha Vikundi vya Vijana na Wanawake katika kufanya shughuli za kiuchumi ili kuondokana na umasikini. Kwa kuzingatia Ibara hizi mbili yafuatayo yamefanyika kutoka mwaka 2015 – 2020.
Mwaka 2015/2016 , mikopo yenye thamani ya Tsh 6,000,000 kwa vikundi 11 (wanawake 6 na vijana 5) , Mwaka 2016/2017, mikopo yenye thamani ya Tsh. 6,000,000/= kwa vikundi 11 (wanawake 6, vijana 5) , Mwaka 2017/2018, mikopo yenye thamani ya Tsh. 15,500,000/=kwa vikundi 31(Wananawake 16, Vijana 14 na Watu wenye Ulemavu 1), Mwaka 2018/2019, mikopo yenye thamani ya Tsh 52,000,000 kwa vikundi35 (Wanawake 17, Vijana 15 na watu wenye ulemavu 3 na kwa mwaka 2019/2020 mikopo yenye thamani ya Tsh. 53,583,876 kwa vikundi 27(wanawake 17, Vijana 7, na watu wenye ulemavu 3).
Mafunzo kwa vikundi 35 vya Wanawake 17 vya Vijana 15 na watu wenye ulemavu 3 vyenye wanachama 336 wanawake 192 na vijana 144, Chuo cha sabasaba VRTC watoa mafunzo ya ushonaji kwa vijana 15 ME 11 na KE 4., Shirika la SEMA wametoa mafunzo ya mapishi, ufugaji kuku, upambaji na ususi kwa vijana 296 KE 185 ME 111, Chuo cha VETA wametoa mafunzo kwa vijana wa kiume 98, International beekeeping open school and post primary education (IBOS) wametoa mafunzo ya ufugaji nyuki kwa vijana 20 KE 9 na vijana ME 11 na hivyo kufanya jumla ya watu 765 waliopata mafunzo wakiwepo KE 390 ME 375
Ilongero
Anuani ya Posta: Box 27, Singida
Simu: +25526502252
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.