• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

DC SINGIDA AZINDUA MSIMU WA KILIMO KWA MWAKA 2023/ 2024

Posted on: October 6th, 2023

“Mkakati wa serikali ni kumuondoa mkulima kwenye kilimo cha mazoea na kwenda katika kilimo cha kibiashara”. Hayo yalisemwa na Mhe. Mhandisi Paskasi Muragili Mkuu wa Wilaya ya Singida (wa kwanza kulia) katika siku ya uzinduzi wa msimu wa kilimo uliofanyika tarehe 5 hadi 6 ya mwezi Oktoba, 2023 katika viwanja vya ofisi ya Mtendaji wa kata Ughandi  Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Singida, Muragili amewataka wakulima kubadili fikra katika kilimo na hivyo kuondokana na kilimo cha mazoea na hivyo kujielekeza katika kilimo biashara kwani uwekezaji mkubwa katika sekta ya viwanda unaendana sambamba na uwekezaji katika sekta ya kilimo na hasa kilimo biashara.

Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida wametakiwa kuchangamkia fursa ya msimu wa kilimo kwa kujisajli katika daftari la wakulima kupitia kwa maafisa kilimo waliopo katika kila kata ili waweze kuunganishwa katika tanzidata ya serikali kwa utambuzi na hivyo kuweza kufkiwa kwa urahisi na kutatua changamoto zinazowakabili kulingana na maeneo yao, pia waweze kupata pembejeo za kilimo kwa bei elekezi ya ruzuku kupitia mawakala wa pembejeo za kilimo wanaotambulika na serikali. Ikumbukwe kuwa katika wilaya ya Singda mvua huanza kunyesha mwishoni mwa mwezi Novemba na kushia mwezi April kila mwaka.







Akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Bi: Natalia Mosha ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida amesema lengo kuu la uzinduzi wa msimu wa kilimo ni kutoa uhabarisho kwa wakulima juu ya kuanza kwa msimu wa shughuli za kilimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Bi Natalia amesema kupitia uzinduzi wa msimu wa kilimo wakulima wtahamasika kuanza kwa shughuli mbalimbali za kilimo ikiwa ni pamoja na kujiandikisha kwenye daftari la ruzuku la mbolea (TFRA), maandalizi ya mashamba, zana za kilimo, mbegu na pembejeo za kilimo.

Katika msimu wa kilimo kwa mwaka 2023/ 2024 Halmashauri ya Wilaya ya Singida imelenga kulima hekta 114,509 ya mazao ya chakula, hekta 6151.2 ya mazao jamii ya mikunde, hekta 65,776.5 ya mazao ya biashara, hekta 854 ya mazao ya mboga mboga na hekta 87.6 ya mazao ya matunda; Hivyo Halmashauri inatarajia kuvuna kiasi cha tani 182,292 kwa mazao ya chakula, tani 7096 kwa mazao jamii mikunde, tani 124,577 kwa mazao ya biashara, tani 602.8 kwa mazao mboga mboga na tani 99.1 kwa mazao ya matunda.

Akizindua mabanda ya utoaji elimu ya kilimo bora na pembejeo za kilimo Mhe. Mhandisi Paskasi Muragili na Mkuu wa Wilaya ya Singida amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida kuhakikisha viongozi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida kuanzia ngazi ya kitongoji hadi kata kulima mashamba darasa katika maeneo walau nusu hekari ili iwe mfano kwa wakulima wanaowasimamia kuiga na kujifunza.

Aidha Mhe. Muragili ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uwekezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Singida katika sekta ya afya, elimu, barabara, umeme, maji, uwezeshaji wa vijana kiuchumi kupitia mikopo ya asilimia 10, na sekta ya kilimo pamoja na kilimo cha umwagiliaji.




Uzinduzi wa msimu wa kilimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida umeambatana na zoezi la kumsajili mkulima katika tanzidata ya Serikali, maonesho ya pembejeo bora za kilimo na viwatilifu yaliyoambatana na utoaji wa mada mbalimbali za kilimo bora na matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo na viwatilifu kwa kilimo biashara yaliyokuwa yakitolewa na wataalamu wa kilimo kutoka mashirika ya Bayers wanaohusika na uzalishaji na usambazaji wa mbolea aina ya Booster, mbegu bora pamoja na viwatilifu; pia mtaalamu wa kilimo kutoka mradi wa Mkulima mbunifu unaosimamiwa na shirika la kilimo endelevu (SAT) wakishirikiana na maafisa kilimo wa Wilaya ya Singida.

Matangazo

  • TANGAZO LA MARUDIO NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA July 02, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA UFADHILI WA MAFUNZO YA KUJENGEWA UWEZO KWA WATUMISHI WA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI July 02, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA KUHU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE NGAZI YA MKOA NA WILAYA KWA MWAKA 2025 June 10, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • ZIARA YA DC GODWIN GONDWE, KUKAGUA MAANDALIZI YA UJIO WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, SINGIDA DC.

    June 21, 2025
  • WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO WA USIMAMIZI WA UTENDAJI KAZI KATIKA UTUMISHI WA UMMA (PEPMIS)

    June 20, 2025
  • TASWIRA YA DARAJA LA JP MAGUFULI, (KIGONGO - BUSISI)

    June 19, 2025
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA DARAJA LA JP MAGUFULI (KIGONGO - BUSISI)

    June 19, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.