• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

HALMASHAURI YA SINGIDA YAANDAA KIKAO CHA WADAU WA UVUVI KUJADILI USALAMA WA WAVUVI NA KUONGEZA MAPATO YA SAMAKI

Posted on: December 30th, 2024

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Mhe.Elia Digha akishirikiana na Kaimu Mkurugenzi Bi.Janeth Mbugha, ameongoza kikao cha wadau wa uvuvi kilichowakutanisha madiwani, viongozi wa wavuvi, wenyeviti na watendaji wa kata na vijiji vinavyozungukwa na mabwawa ya samaki na wataalamu wa Idara ya uvuvi na Timu ya mapato ya Halmashauri.Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 30/12/2024 katika Ukumbi mkubwa uliopo katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Singida,kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali kuhusiana na shughuli za uvuvi,hususan suala la ukusunyaji wa mapato yatokanayo na uvuvi wa samaki.

Akifungua kikao hicho  Mhe.Elia Digha amewasisitiza wenyeviti na watendaji  wa vijiji na kata,kutambua uongozi wa wavuvi kwa kuwasajili wavuvi wote na kuwajua wageni wanaoingia katika vijiji vyao kwaajili ya shughuli za uvuvi ili iwe rahisi kudhibiti vitendo vya kihalifu kwa kuwatambua wahalifu na kuwakamata.

“ Kuna wavuvi wageni ambao wanaenda kila mahali,hivyo watu kama hawa wanaofanya mzunguko mkubwa ni lazima pia tujiridhishe kwa kutambua uongozi wa wavuvi,tukawajua wavuvi wote na usajili wao wote,maana wapo wasio na nia njema ambao wanafanya uhalifu huko, wanakuja kujificha kwenye maeneo yetu ya uvuvi,hivyo anapokuja mgeni tujue huyu ni mgeni kaja, tujuane ili twende vizuri.” Alisema Mhe.Digha.

Pamoja na hayo, wavuvi hao na viongozi wao wa kata na vijiji walipata nafasi ya kuwasilisha changamoto zao na kupatiwa majibu katika kuongeza ufanisi wa kazi zao za uvuvi na ukusanyaji wa mapato ya samaki.

Vilevile katika kikao hicho yaliazimiwa masuala kadha wa kadha,yaliyotolewa kwa wadau wote walihudhuria kikao hicho,ambapo kila mmoja kwa nafasi yake alisisitizwa kutimiza wajibu wake katika kuhakikisha  ukusanyaji wa mapato ya samaki unaongezeka.Maazimio hayo ni kama,matumizi ya Life Jacket ( koti la kuokoa) kwa wavuvi wote katika kujihakikishia usalama wao wawapo katika shughuli zao za uvuvi,uundwaji wa vikundi vya wavuvi vinavyokopesheka, kuacha matumizi ya nyavu haramu za kuvulia samaki kwa lengo la kulinda mazalia ya samaki,na pia Maafisa wa serikali watengeneze urafiki na wavuvi ili kurahisisha ukusanyaji wa mapato ya samaki.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 17, 2025
  • MAENEO YA UWEKEZAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA January 03, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI ZA MUDA July 17, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA PESA ZA MIRADI YA MAENDELEO SEPT 2023 October 18, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA SINGIDA WAPATA MAFUNZO KUHUSU USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KATIKA UWEKEZAJI

    April 03, 2025
  • TAWA YATOA ELIMU YA MBINU ZA KUKABILIANA NA WANYAMA PORI

    April 03, 2025
  • HALMASHAURI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI WATEMBELEA HALMASHAURI YA SINGIDA

    March 28, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AWAASA WALIMU KUEPUKA MIKOPO UMINZA

    March 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.