• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA YAADHIMISHA SIKU YA MNYAMAKAZI PUNDA KWA KUPAZA SAUTI YA USTAWI NA HAKI ZA WANYAMA

Posted on: July 30th, 2025

Halmashauri ya Wilaya ya Singida kupitia Jukwaa la Mnyama Kazi Punda, leo imefanya Maadhimisho ya siku ya mnyamakazi Punda, ikiwa na lengo la kupaza sauti ya utetezi wa wanyama hao na kuhakikisha wafugaji, watumiaji wa Punda na Jamii wanakuwa na uelewa mpana juu ya ustawi wa wanyama hao.

Hafla hiyo iliyofanyika katika kijiji cha Kinyamwenda, Kata ya Itaja, pia imehusisha maadhimisho ya miaka 3 hadi 6 ya utekelezaji wa Mradi wa Ustawi wa Mnyama Kazi Punda, ambao unatekelezwa na Shirika la Inades Formation Tanzania (IFTz), na kufadhiliwa na Brook East Africa kutoka nchini Kenya.Mradi  huu unafanya kazi na vikundi 14 vya wafugaji na watumiaji wa Punda vyenye jumla ya wanachama 240 kutoka katika vijiji vitatu katika Halmashauri, ambavyo ni Endeshi, Ghata na Kinyamwenda.

Akisoma Risala kwa Mgeni rasmi, mbele ya Wananchi na Wageni waliohudhuria, Ndg. John Mwiru ambaye ni muwakilishi wa vikundi hivyo, alisema kwa kipindi cha miaka 3 hadi 6 ya utekelezaji wa mradi, Jukwaa la Mnyama Kazi Punda limekuwa na mafanikio mengi ikiwemo; kutoa elimu ya ustawi wa mnyamakazi Punda kwa wafugaji, watumiaji wa Punda na wanajamii takribani 4,500, kupungua kwa vitendo vya ukatili walivyokuwa wakifanyiwa Punda kama kubeba mizigo bila kuweka tandiko na kufanyishwa kazi bila kujali muda wa kupumzika.

Akijibu risala hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Bw. Christopher Kidubo alieleza namna ambavyo Halmashauri itahakikisha suala la ustawi wa mnyamakazi Punda linazingatiwa.

“ Halmashauri itahakikisha inasimamia sheria ya ustawi wa wanyama, sura 154 ya mwaka 2023 inayotambua haki za wanyama, pia Halmashauri kwa kuwatumia wataalamu wake wa mifugo na maendeleo ya jamiii tutaendeleza juhudi za matumizi bora ya yoki na matandiko ili kumuepusha Punda asipate majeraha na pia tunaahidi sisi Halmashauri kwa kushirikiana na TARI, watafanya utafiti ili tuweze kupata mbegu bora kwaajili ya malisho ya Punda” Alisema Kidubo.

Maadhimisho hayo yalipambwa kwa burudani mbalimbali kama Ngoma, Mashahiri, Maigizo na kucheza Muziki na vilevile yaliongozwa na Kauli mbiu isemayo, “Ustawi wa mnyamakazi Punda ni dhamana yetu na dhamana ya Viongozi”.

Matangazo

  • TANGAZO LA MARUDIO NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA July 02, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA UFADHILI WA MAFUNZO YA KUJENGEWA UWEZO KWA WATUMISHI WA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI July 02, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA KUHU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE NGAZI YA MKOA NA WILAYA KWA MWAKA 2025 June 10, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAFAANYAKAZI NA WANANCHI WAJUMUIKA KATIKA BONANZA LA MICHEZO ILONGERO

    August 09, 2025
  • MSIMAMIZI WA UCHAGUZI SINGIDA ATOA WITO KWA WASAIDIZI KUZINGATIA MAELEKEZO YA MAFUNZO

    August 06, 2025
  • UFUNGUZI WA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI, KWA NGAZI YA KATA

    August 04, 2025
  • MKOA WA SINGIDA WAWEKA MIKAKATI KUKOMESHA VIFO VYA AKINA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA

    July 31, 2025
  • Angalia zote

Video

MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI NA UNYANYASAJI KWA JAMII KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.