• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

HOSPITALI YA WILAYA YA SINGIDA YAPOKEA VIFAA TIBA.

Posted on: April 30th, 2025

Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania(TUGHE), kikishirikiana na Taasisi ya Doris Mollel(Doris Mollel Foundation), wametoa msaada wa vifaa tiba kwaajili ya Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati yaani  Njiti, leo Tarehe 30/4/2025 katika Hospitali ya Wilaya ya Singida.


Akikabidhi vifaa hivyo, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha TUGHE Taifa, Dkt. Jane Madete ameshukuru uongozi wa Halmashauri kwa kuwapokea, na kutoa rai kwa wafanyakazi kuendeleza ushirikiano huu. 

“ Nichukue nafasi hii, kushukuru kwanza kwa kutupokea, tumekuja kuhamasisha na ndio ikaleta fursa hii, msingeweza kutupokea pengine hii fursa isingepatikana kwahiyo huu undugu tulioutengeneza baina ya wafanyakazi wa Halmashauri hii pamoja na sisi chama cha TUGHE uendelee. Tukitengeneza solidarity ya pamoja, tutapata matokeo mazuri na manufaa mengi zaidi, haya ni machache tu.” Alisema Dkt. Jane Madete.



Akipokea vifaa hivyo Kaimu Mkurugenzi, Ndg. Christopher Kidubo, amewashukuru TUGHE na Taasisi ya Doris Mollel kwa vifaa walivyotoa na kutoa rai kwa wadau hao kuendelea kusaidia kwa sababu uhitaji bado upo.

“ Tunawashukuru sana kwa kutuletea msaada huu, kwetu sisi hapa tulikuwa hatuna kabisa Phototherapy, Suction Pump Machine tulikuwa nazo mbili tumeongezewa tatu, lakini Oxygen Concentrator tulikuwa nazo mbili tumeongezewa moja, na tumepewa Baby Coat tano ambazo hatukuwa nazo kabisa. Lakini ndugu Katibu Mkuu na Doris Foundation, uhitaji bado upo, tunaomba kwa ridhaa yako utatusaidia tuweze kupata Patient Monitor pamoja na Room Heater.” Alisema Ndg. Kidubo.



Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na vitanda vya kujifungulia akina Mama wajawazito, Vitanda vya kulalia watoto, mashine za kupumulia watoto, mashine za kidijitali za kupima uzito, mirija ya kupitishia maziwa ya mtoto kwenda tumboni pindi anaposhindwa kunyonya, na mashine za kuwatibia watoto wenye ugonjwa wa homa ya Manjano. Vifaa vyote hivi vimegharimu Shilingi Milioni 7,450,000/=.


Matangazo

  • TANGAZO LA MARUDIO NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA July 02, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA UFADHILI WA MAFUNZO YA KUJENGEWA UWEZO KWA WATUMISHI WA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI July 02, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA KUHU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE NGAZI YA MKOA NA WILAYA KWA MWAKA 2025 June 10, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • ZIARA YA DC GODWIN GONDWE, KUKAGUA MAANDALIZI YA UJIO WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, SINGIDA DC.

    June 21, 2025
  • WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO WA USIMAMIZI WA UTENDAJI KAZI KATIKA UTUMISHI WA UMMA (PEPMIS)

    June 20, 2025
  • TASWIRA YA DARAJA LA JP MAGUFULI, (KIGONGO - BUSISI)

    June 19, 2025
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA DARAJA LA JP MAGUFULI (KIGONGO - BUSISI)

    June 19, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.