• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

KAMATI YA SIASA MKOA YAMTAKA MKANDARASI WA MAJI KIJIJI CHA MUGHUNGA KUKAMILISHA MRADI KWA WAKATI

Posted on: July 25th, 2023

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Mhe. Martha Mlata leo ameiongoza Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Singida pamoja na Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini  Mhe. Ramadhani Ighondo na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Aysharose Matembe kutembelea Miradi  ya Maendeleo ndani ya Halmashauri ya Singida ambapo ameweza kufika na kujionea Mradi wa Maji Kijiji cha Mughunga, Mradi wa ukamilishaji wa Bweni Shule ya Sekondari Mughunga,Mradi wa Ushonaji wa Kikundi cha Maendeleo vijana Mgori na Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Minyaa katika kata ya Kinyeto.

Akiongea baada ya kusomewa taarifa ya mradi katika mradi wa maji kijiji cha Mughunga Mhe. Mlata amemuomba Mkandarasi wa Mradi huo  Ndg Shirima(Universal Construction Ltd) kuongeza kasi ya ukamilishaji wa mradi ili kuweza kuwawezesha wananchi wa kijiji hicho kupata maji safi na salama katika muda walioahidiwa.




Akiwasilisha taarifa ya Ujenzi wa Bweni Shule ya Sekondari Mughunga ,Mkuu wa Shule ya Sekondari Mughunga Ndg Emmanuel Kitiku amesema Shule ilipokea jumla ya Shlingi milioni 30 kwa ajili ya ukamilishaji wa Bweni ambapo mradi huu ulilenga katikakuleta manufaa ya kuinua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi hasa wanaotokea umbali mrefu,kupunguza mdondoko wa wanafunzi na utoro wa rejareja,kuondoa adha ya wanafunzi kukosa nyumba za kuishi na kuboresha mazingira ya Shule ambapo mpaka sasa wameshatumia shilingi milioni 30 kwa kazi hiyo ingawaje bado haijakamilika kwa asilimia miamoja.Akipokea taarifa hiyo Mhe. Mlata amemuagiza Mkurugenzi mtendaji kufanya tathimini ya mapungufu yaliyoko na kuyawasilisha Mkoani kwa ajili ya kuweza kupatiwa ufumbuzi ili wanafunzi waanze  kutumia bweni hilo mapema iwezekanavyo.




Kwa upande wa Mradi wa Vijana Mgori ,Msoma Taarifa Ndg Zaina Abubakari amemuomba Mhe Mwenyekiti wa CCM Mkoa kuwasaidia kupunguza deni la Mkopo uliobaki (kiasi cha shilingi laki saba) ambao Kikundi kilikopeshwa(kikundi kilichukua kiasi cha shilingi milioni mbili na laki tano)  ili kiweze kujipanua zaidi na kutoa elimu ya ushonaji kwa kinamama wengi zaidi.Kwa kuguswa na maombi hayo Mhe. Mlata amefanya harambee fupi na kufanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi laki mbili ambazo amekabidhi kwa kikundi hukuakiwahimiza kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.




Akihitimisha Ziara katika Mradi wa Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Minyaa Mhe. Mwenyekiti wa CCM mkoa amewasisitiza Watendaji wote wa Mradi huo kuhakikisha kuwa unakamilika kwa wakati na kukabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa tayari kwa ufunguzi rasmi.

Matangazo

  • TANGAZO LA BVR May 11, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 17, 2025
  • MAENEO YA UWEKEZAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA January 03, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI ZA MUDA July 17, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA SINGIDA WAPATA MAFUNZO KUHUSU USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KATIKA UWEKEZAJI

    April 03, 2025
  • TAWA YATOA ELIMU YA MBINU ZA KUKABILIANA NA WANYAMA PORI

    April 03, 2025
  • HALMASHAURI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI WATEMBELEA HALMASHAURI YA SINGIDA

    March 28, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AWAASA WALIMU KUEPUKA MIKOPO UMINZA

    March 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.