• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

KIKAO MAALUMU CHA BARAZA LA MADIWANI CHA KUPITIA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA HOJA ZA CAG

Posted on: June 22nd, 2023

Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Peter Joseph Serukamba amehudhuria kikao maalumu cha baraza la madiwani cha kupitia taarifa ya utekelezaji wa hoja za Mdhibiti na Mkaguzi  Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG kwa mwaka wa fedha 2021/ 2022 kilichofanyika leo tarehe 20 Juni, 2023 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ilongero iliyopo katika kata ya Ilongero  Wilaya ya Singida.

Ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Singida katika kuendelea kupunguza hoja za ukaguzi kwa asilimia 50; hata hivyo amekitaka kitengo cha manunuzi ya umma cha Halmashauri  kuongeza umakini katika kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za manunuzi ya umma pamoja na utunzaji wa nyaraka ili kuepukana na hoja zisizo za msingi.

Akiongea katika kikao cha baraza la madiwani Mhe. Serukamba ameipongeza halmashauri katika kuendelea kukabiliana na changamoto za ukusanyaji wa mapato kwani Halmashauri ya Wilaya ya Singida  kwa mwaka wa fedha 2022/ 2023 imekusanya mapato kwa 88% na hadi kufikia mwisho wa mwaka wa fedha halmashauri inatarajia kuvuka zaidi ya lengo waliojiwekea la  100%. Hata hivyo Mhe. Mkuu wa mkoa wa Singida amelishauri baraza la madiwani kubuni na kuongeza vyanzo vipya vya mapato ya halmashauri mbali na kuendelea kutegemea  vyanzo vya mapato ya mazao ya kilimo ambapo kijiografia ukanda wa Singida umekuwa ukitegemea msimu mmoja wa mvua kwa mwaka.  

Amelishauri baraza kutenga maeneo ya mabonde ili kufanya kilimo cha umwagiliaji walau misimu mitatu kwa mwaka ili  kutengeneza ajira kwa vijana na kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya halmashauri.

Akiongelea juu ya chanzo kipya cha kukusanya mapato kupitia usafi na utunzaji mazingira hasa kwa maeneo ya halmashauri yanayoendelea  kwa kasi, Mhe. Serukamba ameishauri halmashauri ya Wilaya ya Singida kupitia baraza la madiwani kutunga sheria ndogo ndogo zitakazowabana wananchi kutotupa uchafu hovyo kwani vifaa vya kukusanyia taka (dustbin) zimewekwa kwa baadhi ya maeneo ya stendi na sokoni.

Mkuu wa mkoa wa Singida ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Singida kuhakikisha ifikapo Juni, 28, 2023 iwe imekamilisha majengo  ya madarasa yanayojengwa kwa mradi wa Boost. Aidha ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwekeza  miradi ya maendeleo ya jamii katika mkoa wa Singida.

Aidha mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida na diwani wa kata ya Msange Mhe. Eliah Digha amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Peter Joseph Serukamba kuwa baraza limepokea maelezo na ushauri wa kiutendaji na kumuhakikishia kufanyia kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.

Mwisho, Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida alimkaribisha Katibu Tawala (DAS) mpya wa Wilaya ya Singida Mhe. Goodluck Abinala Mangomango (wa kwanza kulia kwa meza kuu) kujitambulisha na kusalimia baraza.

Matangazo

  • TANGAZO LA BVR May 11, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 17, 2025
  • MAENEO YA UWEKEZAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA January 03, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI ZA MUDA July 17, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA SINGIDA WAPATA MAFUNZO KUHUSU USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KATIKA UWEKEZAJI

    April 03, 2025
  • TAWA YATOA ELIMU YA MBINU ZA KUKABILIANA NA WANYAMA PORI

    April 03, 2025
  • HALMASHAURI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI WATEMBELEA HALMASHAURI YA SINGIDA

    March 28, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AWAASA WALIMU KUEPUKA MIKOPO UMINZA

    March 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.