• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRICA KWA MWAKA 2023

Posted on: June 19th, 2023

Maadhimisho ya Siku ya  Mtoto wa Africa katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida yamefanyika tarehe 16 Juni, 2023 kwenye viwanja vya ofisi ya Mtendaji wa kata ya Mtinko wilayani Singida chini ya Kauli Mbiu isemayo “Zingatia Usalama wa Mtoto katika Ulimwengu wa Kidigitali”.

Akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Bi. Sylvia Mugasha ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Singida amewahimiza wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuendelea kuwalinda watoto kwani watoto wote wana haki sawa na wanastahili kusikilizwa, kutunzwa, kuendelezwa na kuhudumiwa ipasavyo ili waweze kutimiza ndoto zao.

“Watoto wanahitaji kulindwa dhidi ya ukatili, ubakaji, ndoa katika umri mdogo, uonevu, unyanyasaji na kulindwa dhidi ya matumizi mabovu ya vifaa vya kidigitali ambavyo kimsingi hutoa maudhui yanayopelekea kuvunjika kwa maadili ya mtoto na hivyo kumuharibu kisaikolojia, watoto wanahitaji pia kuendelezwa kwa kupatiwa elimu bora kuanzia elimu ya msingi hadi elimu ya juu ”, alieleza Mugasha.

 Hata hivyo Bw. Ezekiel Mpina ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida ameelezea jitihada zinazofanywa na Halmashauri katika kumlinda mtoto dhidi ya ukatili wa kijinsia. 

“Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida umekuwa ukishirikiana bega kwa bega na wadau wa maendeleo ambao ni Action-Aid, MEDO, ESTL, SAPAWA na SEMA katika kupinga na kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa watoto kwani elimu inayotolewa ya kupinga ukatili wa kijinsia imesaidia kwa kiwango kikubwa katika kubadili mtizamo hasi na fikra potofu ili kuwalinda watoto wote dhidi ya mila na desturi zenye kuwaletea madhara ambazo hapo awali zilikuwa zikipelekea watoto kukatisha masomo”, alieleza Mpina.




Mwakilishi wa Afisa Elimu- Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida mwalimu Antony Kibuga amewahimiza wazazi na walezi kuendelea kuchangia vyakula mashuleni ili watoto waendelee kupata chakula na hivyo kumlinda mtoto awapo katika masomo na kumuwezesha kufikia ndoto zake.

Mwakilishi wa Dawati la Jinsia kutoka Jeshi la Polisi katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida Inspekta Saguda amewataka wazazi, walezi na wananchi wote kwa ujumla kutoa taarifa haraka ya vitendo viovu wanavyofanyiwa watoto kwa mamlaka husika ili kumlinda mtoto chini ya kauli mbiu isemayo “Zingati a usalama wa mtoto katika ulimwenguwakidigitali”.Hata hivyo Inspekta Saguda amewataka wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwasafirisha watoto wa kike mikoani kwenda kufanya kazi za ndani; sambamba na hilo amekemea vikali tabia ya wazazi kuwaozesha watoto wa kike wakiwa na umri mdogo.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE NGAZI YA MKOA NA WILAYA KWA MWAKA 2025 June 10, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA KUHU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 17, 2025
  • MAENEO YA UWEKEZAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA January 03, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • ZIARA YA DC GODWIN GONDWE, KUKAGUA MAANDALIZI YA UJIO WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, SINGIDA DC.

    June 21, 2025
  • WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO WA USIMAMIZI WA UTENDAJI KAZI KATIKA UTUMISHI WA UMMA (PEPMIS)

    June 20, 2025
  • TASWIRA YA DARAJA LA JP MAGUFULI, (KIGONGO - BUSISI)

    June 19, 2025
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA DARAJA LA JP MAGUFULI (KIGONGO - BUSISI)

    June 19, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.