• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

MIRADI NANE YENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 500 IMEPATA BARAKA ZA VIONGOZI WAKIMBIZA MWENGE KITAIFA

Posted on: September 25th, 2023

Miradi nane yenye thamani ya zaidi ya Milioni 500 katika Wilaya ya Singida imepata Baraka za Viongozi wakimbiza Mwenge Kitaifa wanaoongozwa na Kiongozi wao Ndugu Abdallah Shaibu Kaim.

Mwenge wa Uhuru umepokelewa tarehe 24 Septemba 2023 katika viwanja vya kijiji Nkwae, Wilaya ya Singida ukitokea Wilaya ya Mkalama ambapo umetembelea na kukagua miradi nane katika sekta ya  Afya, Maendeleo ya Jamii, Elimu pamoja na Hifadhi ya Mazingira.

Miradi hii ambayo imetembelewa na kukaguliwa na Viongozi wakimbiza Mwenge Kitaifa katika Wilaya ya Singida ni pamoja na mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa Kata ya Kijota, Mradi wa kutengeneza maji tiba katika Hospitali ya St. Calorus Mtinko, Mradi wa Ukarabati wa Ofisi ya kijiji Nduu Kata ya Kijota, Mradi wa Kizimba cha Taka na Barabara  Kata ya Ilongero, Mradi wa Kikundi cha Vijana Kata ya Mwasauya, Mradi wa Josho la Mifugo Mipilo Kata ya Maghojoa na Mradi wa Upandaji miti Mangida Kat ya Msange.Pia programu za Lishe, Malaria, Ukimwi na Madawa ya Kulevya zilitembelewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2023. Miradi yote ya iliyotembelewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge ilikubaliwa na kupata baraka za kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 na kupelekea Halmashauri ya Wilaya ya Singida kuwa Miongoni mwa Halmashauri zilizopata Hati Safi(Clean Sheet) kutoka kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023.

Akiongea na Wananchi wa wilaya ya Singida, Ndugu Abdalah Shaibu Kaim katika ujumbe wake wa Mwenge wa Uhuru amesisitiza jamii kuweka mkazo, kuzingatia na kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya Rushwa, Madawa ya Kulevya, Ugonjwa wa Malaria, Maambukizi mapya ya VVU na ugonjwa wa UKIMWI, na kuzingatia ulaji wa lishe bora katika maisha yetu ya kila siku. Vilevile Ndugu Abdalah ameeleza kwa kina sana juu ya umuhimu wa Watanzania kuweka kipaumbele suala la athari za kimazingira zinazotuathiri kila siku kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo chanzo kikubwa ni uharibifu wa mazingira kwa shughuli zetu za kibinadamu za kila siku kama kilimo pembezoni mwa vyanzo vya maji, ufyekaji misitu hovyo, ufugaji wa mifugo mingi kihorela bila kufuata taratibu na kanuni za ufugaji bora na salama. Hivyo ameiasa sana Jamii ya Wakazi wa Singida kuzingatia umbali wa vyanzo vya maji kwenye shughuli za kilimo, kuzingatia ufugaji bora unaofuata kanuni, lakini pia na kutunza misitu yetu ya asili ikiwa sambamba na kutekeleza maagizo ya Serikali ya kupanda miti kwa wingi na hasa amekumbusha Halmashauri jukumu la kupanda miti milioni moja na nusu kila mwaka.

Ndugu Abdalah kwa niaba ya Wakimbiza Mwenge Kitaifa wengine alioambatana nao, amewashukuru sana wakazi wa Wilaya ya Singida kwa kujitokeza kwa wingi kuja kuupokea Mwenge wa Uhuru na amefurahishwa sana na mapokezi mazuri amabyo vilevile yameenda sambamba na miradi mizuri  na yenye tija kwa maendeleo ya Nchi.

Matangazo

  • TANGAZO LA BVR May 11, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 17, 2025
  • MAENEO YA UWEKEZAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA January 03, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI ZA MUDA July 17, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA SINGIDA WAPATA MAFUNZO KUHUSU USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KATIKA UWEKEZAJI

    April 03, 2025
  • TAWA YATOA ELIMU YA MBINU ZA KUKABILIANA NA WANYAMA PORI

    April 03, 2025
  • HALMASHAURI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI WATEMBELEA HALMASHAURI YA SINGIDA

    March 28, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AWAASA WALIMU KUEPUKA MIKOPO UMINZA

    March 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.