• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

NIMESAINI NOTISI ZA KUVUNJA MABARAZA YA MADIWANI - MCHENGERWA

Posted on: June 16th, 2025

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kwa kuzingatia mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa sheria, tayari amekwisha saini notisi za kuvunjwa kwa Mabaraza ya Madiwani katika Mamlaka za Wilaya na Mamlaka za Miji, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.Waziri Mchengerwa amesema hayo leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI jijini Dodoma.


Mhe. Mchengerwa amesema kuwa, notisi hizo za kuvunjwa kwa Mabaraza ya Madiwani katika Mamlaka za Wilaya, na Mamlaka za Miji, 2025 zitatangazwa kwenye Gazeti la Serikali hivi karibuni.Mhe. Mchengerwa amefafanua kuwa, notisi hizo zinaelekeza kwamba vikao vya Halmashauri na Kamati zake zinapaswa ziwe zimekoma siku saba kabla ya kuvunjwa kwa Bunge hapo tarehe 27 Juni, 2025.

“Vikao vya Halmashauri na Kamati zake zinapaswa kuwa zimekoma ifikapo tarehe 20 Juni, 2025 hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri atawajibika kwa kufanya kikao chochote cha Halmashauri au Kamati yake baada ya tarehe hiyo,” Waziri Mchengerwa amesisitiza.


Baada ya mabaraza ya madiwani kufikia ukomo tarehe 20 Juni 2025, Mhe. Mchengerwa ameelekeza masuala yote ya kiutendaji katika Halmashauri kusimamiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri, ambaye atakuwa Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kipindi cha mpito, akisaidiana na Wakuu wa Idara watakaokuwa kama wajumbe wa kamati.

Sanjari na hilo, Waziri Mchengerwa ameelekeza kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hataruhusiwa kuanzisha miradi au uwekezaji mpya ikiwa ni pamoja na kubadilisha au kurekebisha mradi, uwekezaji au uamuzi wowote uliopitishwa na Halmashauri kabla ya kuvunjwa.

“Matumizi mabaya ya mamlaka au kutotekeleza kwa ufanisi majukumu ya kiutawala kwa mujibu wa notisi hizi, kutamfanya Mkurugenzi kuwajibika binafsi kwa mujibu wa Sheria,” Mhe. Mchengerwa amehimiza.


Pia, Waziri Mchengerwa ameelekeza kwamba katika kikao cha kwanza cha Baraza jipya la Madiwani baada ya uchaguzi kufanyika, Mkurugenzi wa Halmashauri atapaswa kuwasilisha taarifa ya maamuzi na mwenendo wa vikao vya menejimenti vilivyofanyika wakati wa kipindi cha mpito.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUKODISHWA KWA SHAMBA LA MBEGU LA MPAMBAA September 16, 2025
  • TANGAZO LA WATUMISHI KUHUSU WCF September 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI August 30, 2025
  • TANGAZO LA FURSA ZA KUTOA HUDUMA ZA CHAKULA (CATERING) KATIKA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA September 01, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MKUTANO MAALUM WA MAANDALIZI YA MSIMU WA KILIMO, WILAYA YA SINGIDA.

    October 03, 2025
  • TIMU YA UKAGUZI KUTOKA KIKOSI CHA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, YAFANYA UKAGUZI.

    October 02, 2025
  • MHE. GONDWE ATEMBELEA MIRADI YA LISHE KATIKA SHULE 3 ZA SEKONDARI.

    September 29, 2025
  • USAFI WA MAZINGIRA WAFANYIKA, KATA YA MUGHAMO

    September 26, 2025
  • Angalia zote

Video

WATUMISHI WAPYA WAASWA KUWEKA AKIBA
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.