Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge leo amekabidhi pikipiki 166 kwa Maafisa Ugani wa Halmashauri za mkoa huo kama sehemu ya vitendea kazi na kuwataka kufanya mabadiliko makubwa kwenye sekta ya kilimo na ufugaji huku akisisitiza upatikanaji wa takwimu sahihi kwa kuwa itakuwa rahisikuwafikia wakulima popote walipo.
Akizungumza kabla ya kukabidhi pikipiki hizo Dkt. Mahenge amesema pikipiki 161 zitakabidhiwa kwa Maafisa Ugani wa Halmashauri za Manyoni, Singida Dc, Iramba, Mkalama na Manispaa ya Singida huku pikipiki tano(5) zikigawiwa kwa Maafisa Ushirika wa Mkoa ambapo zitatumika kuwafikia wakulima pamoja na vyama vya Ushirika katika kuleta tija kwenye Kilimo.
Aidha Dkt Mahenge ameeleza kwamba msimu wa kilimo unaokuja serikali inampango wa kugawa mbegu za allizeti kwa wakulima kama ilivyofanya kwa msimu uliopita hivyo akawaagiza Maafisa Ugani hao kuimarisha usimamizi wa kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo ambayo yatachangia pato la wakulima na taifa kwa ujumla.
Naye Natalia Mosha Afisa Kilimo(W) kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Singida akiishukuru Serikali kwa kuwapatia pikipiki hizo huku akiahidi kwamba wataweza kuwafikia na kuwahudumia wakulima wengi kwa muda mfupi jambo ambalo litaleta matokeo makubwa katika sekta hiyo.
Ilongero
Anuani ya Posta: Box 27, Singida
Simu: +25526502252
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.