• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

SERIKALI YAWAHIMIZA WAFUGAJI MKOANI SINGIDA KULINDA MIFUGO KUPITIA CHANJO NA UTAMBUZI

Posted on: July 8th, 2025

Wafugaji mkoani Singida wametakiwa kushiriki kikamilifu katika zoezi la uchanjaji na utambuzi wa mifugo yao, ambapo utekekelezaji wa zoezi hilo mkoani humo limeanza rasmi leo, Julai 8, 2025, katika Kata ya Kyengege, Kijiji cha Makunda, Wilaya ya Iramba. Lengo la zoezi hilo ni kulinda mifugo dhidi ya magonjwa na kuboresha ubora wake kwa ajili ya ushindani katika soko la kimataifa.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mafunzo ya Mifugo (LITA), Dkt. Pius Mwambene, amesema kuwa zoezi hilo ni sehemu ya kampeni ya kitaifa ya uchanjaji na utambuzi wa mifugo, iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 16 Juni 2025. Amesema kampeni hiyo inalenga kuongeza tija kwa wafugaji nchini, hivyo ni muhimu kulizingatia.

Dkt. Mwambene alieleza kuwa katika kampeni hiyo, wafugaji watanufaika na chanjo kwa gharama ya ruzuku baada ya Serikali kutoa kiasi cha Shilingi Bilioni 216 kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo kwa kipindi cha miaka mitano. "Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alishazindua kampeni hii ya chanjo na ameridhia kuchangia nusu gharama ya chanjo ili kuwasaidia wafugaji kote nchini kuikinga mifugo yao dhidi ya magonjwa na kuimarisha biashara ya Mifugo na mazao yake katika masoko ndani na Kimataifa, hivyo wafugaji wa mkoa huu wa Singida jitokezeni na mshiriki kikamilifu kwenye kampeni hii" alisema Dkt. Mwambene.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Wilaya ya Iramba, Bw. Morton Msowoya, alibainisha aina za chanjo zitakazotolewa ni chanjo dhidi ya homa ya mapafu kwa Ng’ombe, Sotoka kwa Mbuzi na Kondoo, pamoja na chanjo dhidi ya Kideli, Mafua na Ndui. Baadhi ya wafugaji wilayani Iramba wameishukuru Serikali kwa kuwawezesha kupata chanjo kwa ruzuku wakieleza kuwa kabla ya kuanzishwa kwa kampeni hiyo mifugo mingi ilikufa kutokana na magonjwa. Utekelezaji wa zoezi hilo kwa ngazi ya mkoa wa Singida unaenda sambamba na uhamasishaji kwa wafugaji kushiriki kikamilifu, ambapo zaidi ya mifugo milioni 4 inatarajiwa kuchanjwa mkoani Singida.

Matangazo

  • TANGAZO LA MARUDIO NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA July 02, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA UFADHILI WA MAFUNZO YA KUJENGEWA UWEZO KWA WATUMISHI WA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI July 02, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA KUHU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE NGAZI YA MKOA NA WILAYA KWA MWAKA 2025 June 10, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAFAANYAKAZI NA WANANCHI WAJUMUIKA KATIKA BONANZA LA MICHEZO ILONGERO

    August 09, 2025
  • MSIMAMIZI WA UCHAGUZI SINGIDA ATOA WITO KWA WASAIDIZI KUZINGATIA MAELEKEZO YA MAFUNZO

    August 06, 2025
  • UFUNGUZI WA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI, KWA NGAZI YA KATA

    August 04, 2025
  • MKOA WA SINGIDA WAWEKA MIKAKATI KUKOMESHA VIFO VYA AKINA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA

    July 31, 2025
  • Angalia zote

Video

MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI NA UNYANYASAJI KWA JAMII KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.