• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

SINGIDA DC YAUZA TANI LAKI 248 KWA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI

Posted on: September 9th, 2024

Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Bi. Natalia Mosha ametoa wito kwa wakulima wa zao la Dengu wilayani humo kutumia mfumo wa Stakabadhi ya Mazao Ghalani kwani mfumo huo hutoa bei halisi ya soko na kumwongezea kipato zaidi mkulima

Bi. Mosha ameyasema hayo terehe 03/09/2024 katika ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Singida Mwahango Kata ya Ilongero alipokuwa akitoa ufafanuzi wa mauzo ya Dengu yaliofanyika mwishoni mwa mwezi wa nane mwaka 2024 ambapo ameendelea kuwasisitiza wakulima kutumia mfumo wa Stakabadhi Ghalani huku akiahidi kuendelea kutoa elimu kuhusu faida ya mfumo huo kwa wakulima pamoja na namna unavyorahisisha uchangiaji wa mapato kwa Serikali.

“Mfumo upo vizuri kwa upande wa Halmashauri unatusaidia kupata mapato moja kwa moja kwa sababu unajua umeuza kiasi gani na umepata kiasi gani kwa hiyo Halmashauri tunajua kabisa tunapata kiasi gani kwa hiyo inaturahisishia na sisi kupata takwimu zile za kiasi cha Dengu iliyouzwa”

Halmashauri ya Wilaya ya Singida ina jumla ya Maghala makuu mawili  ambayo ni Mtinko na Mwasauya ambapo yanafanya kazi na vituo vya kukusanyia mazao katika kata zifuatavyo; Mtinko, Mudida, Mwasauya, Kinyeto, Msange, Mgori, Ngimu,ambavyo hutumika kukusanya na kusafisha dengu kabla ya kupelekwa katika ghala kuu, kisha mwendesha ghala huandaa Katalogi ya Mauzo ili kunadiwa na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) kila zinapotimia tani 20 au zaidi kwa wakati mmoja.

Naye Abasi Athuman kutoka kata ya Ngimu ambaye ni moja kati ya wakulima walioshiriki mnada wa mwisho wa mwezi wa nane ameshukuru uwepo wa mfumo huo ambao umemsaidia kupunguza gharama za usafirishaji pamoja na kuokoa gharama za ushuru wa zao hilo. Kwa upande wake Salim Juma (Mkulima wa Dengu) kutoka kata ya Mwasauya ameshukuru uwepo wa mfumo kwa sababu ya uwaishwaji malipo kwa mkulima mara baada tu ya mnada huku akitoa ushauri kwa serikali kutangaza mnada kwa haraka ili kusaidia mazao ya mkulima yasikae ghalani kwa muda mrefu na kupelekea kushawishika kuuza nje ya mfumo.

Jumla ya kilo za Dengu laki mbili na elfu arobaini na saba mia sita hamsini na nne (247,654) sawa na  Tani 248 zimeuzwa ndani ya mwezi wa nane mwaka 2024 huku pakiwa na ongezeko la idadi ya wakulima walioshiriki kutumia mfumo wa Stakabadhi ya Mazao Ghalani.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUKODISHWA KWA SHAMBA LA MBEGU LA MPAMBAA September 16, 2025
  • TANGAZO LA WATUMISHI KUHUSU WCF September 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI August 30, 2025
  • TANGAZO LA FURSA ZA KUTOA HUDUMA ZA CHAKULA (CATERING) KATIKA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA September 01, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MKUTANO MAALUM WA MAANDALIZI YA MSIMU WA KILIMO, WILAYA YA SINGIDA.

    October 03, 2025
  • TIMU YA UKAGUZI KUTOKA KIKOSI CHA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, YAFANYA UKAGUZI.

    October 02, 2025
  • MHE. GONDWE ATEMBELEA MIRADI YA LISHE KATIKA SHULE 3 ZA SEKONDARI.

    September 29, 2025
  • USAFI WA MAZINGIRA WAFANYIKA, KATA YA MUGHAMO

    September 26, 2025
  • Angalia zote

Video

WATUMISHI WAPYA WAASWA KUWEKA AKIBA
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.