• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

VIONGOZI WILAYA YA SINGIDA WAPEWA MAFUNZO YA UWASILISHAJI NA UHAMASISHAJI WA MATUMIZI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022

Posted on: July 8th, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Mhandisi Paskas Muragili amefungua Semina ya Uwasilishaji Mafunzo na Uhamasishaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Wilaya ya Singida. Mafunzo hayo yaliyoshirikisha Makundi yote yamefanyika katika Ukumbi wa Mwenge Sekondari uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Singida. Mafunzo haya yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa CCM wilaya, Mbunge wa Singida Kaskazini , Mbunge wa Manispaa ya Singida,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manispaa na Mwenyekiti wa Halmashauri Singida Vijijini,Wajumbe Kamati ya Usalama ya Mkoa,Wajumbe Kamati ya Usalama ya Wilaya Sekretarieti ya Mkoa wakiongozwa na Katibu Tawala Mkoa, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri ya Singida na Manispaa, Wakuu wa Taasisi, Waheshimiwa Madiwani , Wajumbe wa Kamati ya Sensa Wilaya, Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa,Watendaji wa Kata, Vijiji na Mitaa,Watumishi ngazi ya Wilaya na Viongozi wa Dini ngazi ya Wilaya.




Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Mhandisi Paskas Muragili amempongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kufanyika kwa Sensa ya Watu na Makazi ya 2022 ambayo ilifanyika kwa pamoja na Mazoezi mengine Mawili na kuwa imejibu maswali ya maeneo matatu yaani Sensa ya Watu, Sensa ya Makazi na Anwani za Makazi ambapo Mkoa wa Singida ni miongoni mwa Mikoa iliyofanya Zoezi hilo kwa Ufanisi mkubwa. Akiongelea kuhusu hadhara iliyoshiriki mafunzo hayo amesema imebidi kuita makundi yote hayo ya Viongozi na Watendaji kwani ni wajibu wao kwenda kufikisha uhabarisho kwa wananchi walioko chini yao na amewahimiza kuwa baada ya semina hii Viongozi wote wazungumzie matokeo ya Sensa katika mikutano yao ilikusudi wananchi waweze kuelewa na namna nzuri ya matumizi ya matokeo yake.

Nikimnukuu Mkuu wa Wilaya amesema “Ndugu viongozi  na washiriki mafunzo haya ya leo yana umuhimu wa kipekee kwa kuwa yameshirikisha viongozi na watendaji wa ngazi mbalimbali za utawala katika wilaya zetu, ambao kwa namna moja au nyingine tunashiriki katika kufanya maamuzi yanahusiana sana na mipango ya maendeleo ya wananchi wetu kwa upande mwingine ina maana tupo karibu sana na wananchi hivyo tunapojengewa uwezo wa kutumia matokeo ya sense tutakuwa na uwezo mzuri katka kutekeleza majukumu yetu ya kuwawakilisha wananchi na tutakuwa na uwezo mzuri wa kutekeleza majukumu yenu ya kuwatumikia wananchi.”

Mhe. Mhandisi Paskas Muragil ameisitiza  washiriki mafunzo haya yanayoekelezwa kwa mujibu wa mpango kazi wa uusambazaji wa Mafunzo ya Matumizi Bora ya Matokeo ya Sensa 2022 unaotokana na maono ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Kiongozi wetu mpendwa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweza kuhakikisha kuwa anafahamu vyema kutumia matokeo ya sensa katika kufaya maamuzi na kusimamia utekelezaji wa mpango mbalimbali ya maendeleo kwenye maeneo yetu.

Matangazo

  • TANGAZO LA BVR May 11, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 17, 2025
  • MAENEO YA UWEKEZAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA January 03, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI ZA MUDA July 17, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA SINGIDA WAPATA MAFUNZO KUHUSU USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KATIKA UWEKEZAJI

    April 03, 2025
  • TAWA YATOA ELIMU YA MBINU ZA KUKABILIANA NA WANYAMA PORI

    April 03, 2025
  • HALMASHAURI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI WATEMBELEA HALMASHAURI YA SINGIDA

    March 28, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AWAASA WALIMU KUEPUKA MIKOPO UMINZA

    March 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.