• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

WAJASIRIAMALI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA WANUFAIKA NA MAONESHO YA SABA YA MIFUKO NA PROGRAMU ZA UWEZESHAJI WA WANANCHI KIUCHUMI

Posted on: September 15th, 2024

Wajasiriamali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Singida wamepata fursa ya kujifunza na kukuza shughuli zao katika Maonesho ya Saba ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, yaliyoandaliwa na Baraza la taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi yaliyofanyika katika viwanja vya Bombadia, Mkoani Singida.

Maonesho hayo yaliyoongozwa na kauli mbiu “Shiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa, unufaike na fursa za uwezeshaji” yalianza tarehe 08/09/2024 na kuhitimishwa tarehe 14/09/2024 yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, viongozi wa kisiasa, viongozi wa dini, mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali, watendaji wa serikali, wajasiriamali na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza katika hafla ya kuhitimisha maonesho hayo, mgeni rasmi Naibu Waziri Mkuu Mhe. Doto Biteko amepongeza kazi kubwa iliyofanywa na mifuko na programu mbali mbali za uwekezaji katika kuhamasisha wajasiriamali kuwekeza tangu mwanzo wa maonesho.

“Nimepita kwenye mabanda nimeona mlivyojitokeza kwa wingi ……. hii mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi wameeleza hapa kazi walioifanya kutoka mwanzo wa maonesho mpaka sasa wamefanya kazi kubwa na tunawapongeza sana.” Alisema Dkt. Biteko.

Pia Mhe. Dkt. Biteko alisisitiza juu ya ushiriki wa wananchi katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakao fanyika tarehe 27/11/2024 kupitia kauli mbiu ya maonesho hayo.

“Kauli mbiu hii inaongeza hamasa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, unaotarajiwa kufanyika novemba 27 mwaka huu katika mikoa yote hapa nchini………nitumie fursa hii vilevile kuwakumbusha wananchi wote wenye sifa ya kuchaguliwa kushiriki kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa. Napenda kutoa rai kwamba msifanye kosa kuchagua viongozi ambao hawana uchungu na maendeleo yetu na taifa kwa ujumla……uchaguzi huu sio uchaguzi mdogo, ni uchaguzi mkubwa kwa maendeleo ya nchi yetu.”Alisema Dkt. Biteko.

Kwa upande wake Bi Joahilia Nimu, mmoja wa wajasiriamali kutoka kata ya Kinyeto, Halmashauri ya wilaya ya Singida amesema maonesho hayo yamemsaidia kujifunza mambo mbalimbali kuhusiana na shughuli zake za ujasiriamali na yatakuwa msaada mkubwa katika kukuza biashara zake hata kuuza mazao na bidhaa nje ya mkoa wa Singida.

“Tumejifunza ujasiriamali, tumeona bidhaa mbalimbali, na sisi wakulima wa mbogamboga wametupa hamasa ya kulima kilimo chenye tija ili kuleta mafanikio kwa mfano, katika hizo mboga tunapaswa kutumia viuatilifu ili mazao yastawi vizuri, vilevile tunakumbwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa mitaji hivyo tunahitaji kuwezeshwa.” Alisema Bi Joahilia Nimu.

Naye mjasiriamali wa ushonaji wa nguo Bi. Anuarite Constantine ameeleza namna alivyojifunza mitindo mbalimbali ya ushonaji sambamba na matumizi ya machine za kisasa za kushonea nguo.

“Mengi tumejifunza kutoka kwa wenzetu,tumejionea staili mbalimbali za nguo kwa upande wangu mimi kama mshonaji wa nguo na mfumaji wa masweta.” Alisema Bi. Anuarite Constantine.

Maonesho ya nane ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Kiuchumi yanatarajiwa kufanyika mwaka 2025 mkoani Mwanza, ikiwa ni makubaliano kati ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na wawakilishi wa mikoa yote ya Tanzania bara ambao ni marafiki wa uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Matangazo

  • TANGAZO LA MARUDIO NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA July 02, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA UFADHILI WA MAFUNZO YA KUJENGEWA UWEZO KWA WATUMISHI WA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI July 02, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA KUHU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE NGAZI YA MKOA NA WILAYA KWA MWAKA 2025 June 10, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • ZIARA YA DC GODWIN GONDWE, KUKAGUA MAANDALIZI YA UJIO WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, SINGIDA DC.

    June 21, 2025
  • WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO WA USIMAMIZI WA UTENDAJI KAZI KATIKA UTUMISHI WA UMMA (PEPMIS)

    June 20, 2025
  • TASWIRA YA DARAJA LA JP MAGUFULI, (KIGONGO - BUSISI)

    June 19, 2025
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA DARAJA LA JP MAGUFULI (KIGONGO - BUSISI)

    June 19, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.