• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

WAKUU WA WILAYA, SINGIDA NA HANANG WAFANYA ZIARA YA KUANGALIA MIPAKA KATI YA WILAYA HIZO

Posted on: September 23rd, 2024

Mkuu wa wilaya ya Singida Mhe. Godwin Gondwe akishirikia na mkuu wa wilaya ya Hanang Mhe. Almishi Issa wamefanya ziara kazi ya kutembelea Hifadhi ya msitu wa Mgori unaojumuisha kata ya Mughunga na Ngimu zilizopo wilayani Singida pamoja na Lalaji iliyopo wilaya ya Hanang, lengo likiwa ni kuona mipaka halisi ya hifadhi hiyo pamoja na kusikiliza kero za wananchi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi.

Ziara hiyo imefanyika leo Septemba 23, 2024 Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara ikihusisha kamati za usalama, wataalamu wa ardhi wa mikoa yote miwili, madiwani wa kata zote tatu, wenyekiti wa vijiji vinavyopakana na hifadhi hiyo, pamoja na Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida ambao kwa pamoja wamefika uwanadani kuangalia mipaka na kuongea na wananchi kuhusu mgogoro huo.

Akizungumza katika ziara hiyo Mhe. Gondwe amewomba wataalamu wa ardhi wa wilaya zote mbili kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kubainisha mpaka wa Msitu, kutoa elimu kwa wananchi ili kuzitambua sheria za misitu lakini pia ametoa rai kwa wananchi kuwa wavumilivu wakati serikali ikiendelea na utatuzi wa mgogoro huo.

“Mpaka wa msitu ujulikane, sheria za msitu tuzifahamu, tukitaka kubadilisha sasa kwa sababu huu ni mpaka wa msitu na wala sio mpaka wa kimkoa kwa hiyo lazima vigezo na masharti kuzingatiwa muanze michakato midogo midogo  kuanzia chini hadi juu ndio mambo yafanikiwe.” Alisema Mhe. Gondwe

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Hanang Mhe. Almishi Issa amewaomba wataalamu wa ardhi kutumia ujuzi wao kuongoza katika zoezi hilo la utatuzi wa mgogoro huo wa mpaka.

Pia, katika ziara hiyo wananchi wamehamasishwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa ifikapo Novemba 2024.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUKODISHWA KWA SHAMBA LA MBEGU LA MPAMBAA September 16, 2025
  • TANGAZO LA WATUMISHI KUHUSU WCF September 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI August 30, 2025
  • TANGAZO LA FURSA ZA KUTOA HUDUMA ZA CHAKULA (CATERING) KATIKA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA September 01, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MKUTANO MAALUM WA MAANDALIZI YA MSIMU WA KILIMO, WILAYA YA SINGIDA.

    October 03, 2025
  • TIMU YA UKAGUZI KUTOKA KIKOSI CHA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, YAFANYA UKAGUZI.

    October 02, 2025
  • MHE. GONDWE ATEMBELEA MIRADI YA LISHE KATIKA SHULE 3 ZA SEKONDARI.

    September 29, 2025
  • USAFI WA MAZINGIRA WAFANYIKA, KATA YA MUGHAMO

    September 26, 2025
  • Angalia zote

Video

WATUMISHI WAPYA WAASWA KUWEKA AKIBA
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.