• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

WALIMU WA SOMO LA KIINGEREZA WAPATIWA MAFUNZO

Posted on: January 29th, 2025

Walimu wa somo la Kiingereza katika Shule zote 102 za Msingi za Halmashauri ya Wilaya ya Singida wamepatiwa Mafunzo ya kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji wa somo la kiingereza kuanzia  leo tarehe 29/01/2025 katika ukumbi wa kituo cha Walimu Singida. Mafunzo hayo ya siku tatu, yameandaliwa na Serikali kwa kushirikiana  na Mradi wa Shule Bora na kuratibiwa na Idara ya Elimu Msingi ya Halmashauri ya Wilaya ya Singida, na kutolewa na wawezeshaji ambao wanatoka miongoni mwa Walimu hao, wakitumia njia mbalimbali za uwasilishaji, kama, kujadiliana katika makundi na kuonyesha kwa vitendo.Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha Walimu hao kuendana na Mtaala mpya wa somo la kiingereza wa mwaka 2023, ili waweze kujengewa uwezo katika kuwafundisha wanafunzi kwenye Shule zao.

Akitoa salamu kabla ya mafunzo kuanza, Mthibiti ubora wa Elimu, Wilaya ya Singida, Bi.Mary D. Maanga amewashauri Walimu hao kuendelea kuwa kama jumuia ya wasomi wa somo la Kiingereza, ambapo watapata nafasi ya kushirikishana changamoto wanazokumbana nazo katika ufundishaji,ili waweze kusaidiana.

“ Hii ni aina ya jumuia ya wasomi wa kiingereza,hivyo nataka kumtia moyo mratibu wa jumuia hii,kuunda kundi ambalo mtakuwa mkishirikishana changamoto zinazowakabili pindi mnapofundisha somo hili mashuleni kwenu.Nafikiri itakuwa ni jukwaa zuri la kupata usaidizi mzuri,kwani unaweza kuwa na changamoto kwenye eneo fulani na ukapata Mwalimu mwingine ambaye anaweledi katika eneo hilohilo, hivyo utapata usaidizi katika changamoto yako.Kwahiyo, nataka mfanye hili jukwaa kuwa la kudumu kuhusiana na ufundishaji wa somo la kiingereza.” Alisema Bi.Mary, akizungumza kwa lugha ya kiingereza.

Katika Mafunzo hayo Walimu wamepata nafasi ya kujifunza  mada mbalimbali zikiwemo, matumizi ya Teknolojia katika ufundishaji, sifa za Mwalimu bora wa somo la kiingereza na jinsi ya kuwafundisha wanafunzi ili kuwaongezea ujuzi wa matamshi ya lugha hiyo katika namna ya kuzungumza na kusikia, pia kusoma na kuandika.

Matangazo

  • TANGAZO LA BVR May 11, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 17, 2025
  • MAENEO YA UWEKEZAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA January 03, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI ZA MUDA July 17, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA SINGIDA WAPATA MAFUNZO KUHUSU USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KATIKA UWEKEZAJI

    April 03, 2025
  • TAWA YATOA ELIMU YA MBINU ZA KUKABILIANA NA WANYAMA PORI

    April 03, 2025
  • HALMASHAURI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI WATEMBELEA HALMASHAURI YA SINGIDA

    March 28, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AWAASA WALIMU KUEPUKA MIKOPO UMINZA

    March 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.