MAADHIMISHO YA WIKI YA MGONJWA YASIYOAMBUKIZA TAREHE 7 - 14 NOVEMBA 2020
LENGO:
Ni kuhakikisha huduma za Kinga na Tiba zinawafikia wananchi wote ili kukabiliana na Ongezeko la kasi la magonjwa haya katika nchi yetu.
Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni magonjwa ambayo hayasambazwi kwa mtu mwingine kwa kuwa hakuna vimelea mwilini vinavyohusiana na magonjwa hayo. Magonjwa hayo ni kama , Magonjwa ya Moyo , figo saratani , Kifua sugu, Kisukari, Magonjwa ya akili na Selimundu
KUJIKINGA:
- Kula mlo kamili wenye mchanganyiko wa vyakula.
- Kutokutumia mafuta mengi
- Punguza chumvi na Sukari
- Kula matunda na mbogamboga kwa wingi
- Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi
- Kufanya mazoezi
- Epuka Msongo wa Mawazo
- Epuka Tumbaku na Madawa ya kulevya
- Epuka unywaji wa pombe kupita kiasi
Bomani Area
Anuani ya Posta: Box 27, Singida
Simu: +25526502252
Simu ya Mkononi: +25526502237
Barua Pepe: ded@singidadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.