Ndugu Ester Anania Chaula Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Singida (wa kwanza kulia) akiongozana na timu ya Menejimenti ya Watumishi wa Halmashauri hiyo katika kutoa huduma za Kijamii kwa watoto wenye Ulemavu waishio Ilongero Parish iliyopo kata ya Ilongero wilaya ya Singida, kwani watoto hao wanapitia changamoto mbalimbali hasa katika malezi na makuzi ya kimwili na kiakili. Aidha msimamizi wa kituo hicho kinachosimamiwa na Jimbo Katoriki Singida, Sister Maria Gesi (wa kwanza kushoto kwa waliosimama) ameishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kujali na kutoa kipaumbele kwa kundi la watoto wenye ulemavu katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Sherehe za miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Ilongero
Anuani ya Posta: Box 27, Singida
Simu: +25526502252
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.