Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Mhandisi Paskas Muragili (wa tatu kulia) ambaye pia ni mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za maika 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Uhasibu wilayani Singida kwa njia ya mdahalo. Kongamano hilo lilijumuisha wageni waalikwa, viongozi wa dini, wanachuo kutoka vyuo vya Uhasibu, Utumishi wa Umma na chuo cha Maendeleo ya wananchi (FDC) pamoja na Watumishi wa Umma kutoka Halmashauri ya Wilaya Singida na Manispaa ya Singida. Akichangia mada kwenye mdahalo wenye kuhitaji tafakuri ya mafanikio ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Mkuu huyo wa Wilaya ameelezea mafanikio makubwa ambayo nchi ya Tanzania imeyapata katika kipindi cha miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara ikiwemo mafanikio katika sekta ya elimu nchini kuanzia elimu awali hadi elimu ya chuo kikuu, mapinduzi katika sekta ya kilimo na umwagiliaji, pia sekta ya afya, miundombinu na ukuaji mkubwa wa teknolojia ya habari na mawasiliano.
Mhe. Mhandisi Paskas Muragili ameyataja baadhi ya mafanikio ambayo Wilaya ya Singida imeyapata katika kipindi cha miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara ikiwemo sekta ya elimu, kwamba kabla ya Uhuru Wilaya ya Singida ilikuwa na shule za msingi 21 ambapo kwa sasa Wilaya ya Singida inakadiliwa kuwa na zaidi ya shule za msingi 167. Pia kabla ya Uhuru wa Tanzania Bara udahili wa watoto mashuleni katika Wilaya ya Singida ulikuwa chini ya asilimia 25 ambapo hivi sasa udahili umeongezeka kwa zaidii ya asilimia 95 Wilayani humo. Akielezea kundi la watoto wenye mahitaji maalumu Mhe. Muragili amesema kabla ya Uhuru wa Tanzania Bara Wilaya ya Singida haikuwa na shule ya ellimu maalumu, ambapo hivi sasa Wilaya ya Singida ina jumla ya shule 7 za elimu maalumu zenye jumla ya wanafunzi 451. Vivyo hivyo kabla ya Uhuru wa Tanzania Bara Wilaya ya Singida ilkuwa na huduma duni ya upatikanaji wa maji safi na salama ambapo hivi sasa tunashuhudia mafanikio makubwa katika sekta ya maji kupitia Wakala wa Maji Mijini na Vijijini (RUWASA) kwa zaidi ya asilimia 67.4 na hivyo kuchochea uchumi wa viwanda. Akielezea juu ya sekta ya viwanda vidogo vidogo wilayani Singida, Mkuu huyo wa Wilaya ameongezea na kusema kabla ya Uhuru wa Tanzania Bara Wilaya ya Singida haikuwa na viwanda vidogo vidogo ambapo hivi sasa Wilaya ya Singida inakadiliwa kuwa na viwanda vya kati 15 na uwepo wa viwanda vidogo vidogo zaidi ya 221. Katika sekta ya mifugo, kabla ya Uhuru Wilaya ya Singida haikuwa na josho la kuoshea mifugo, ambapo hivi sasa Wilaya ya Singida inakadiliwa kuwa na zaidi ya majosho 36.
Katika kuendelea kutafakari mafanikio ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Mhandisi Paskas Muragili ameitaka jamii ya kitanzania kuendelea kuenzi Tunu za Taifa la Tanzania tulizoachiwa na waasisi wetu Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume kama kauli mbiu ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara isemavyo "AMANI NA UMOJA, NGUVU YA MAENDELEO YETU ". Hata hivyo Mhe. Muragili amewaasa vijana kuwa wazalendo na kuipenda nchi yao kwani tutakaoiharibu ni sisi na tutakaoijenga ni sisi pia; Akisistiza swala la mmomonyoko wa maadili; Mkuu huyo wa Wilaya ya Singida amehimiza vijana wa kitanzania kujiepusha na vitendo viovu na hivyo ameitaka jamii ya kitanzania pamoja na viongozi wa dini kuhubiri somo la uzalendo kwa vijana.
Aidha Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Singida Elia Digha (wa pili kulia) ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutenga fedha za Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara zaidi ya millioni 900 na kuelekeza fedha hizo kujenga mabwalo 8 ya shule za wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Pia ameishukuru Serikali kufanya makongamano ya Mdahalo kutafakari mafanikio ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara na hivyo kupata dila ya maendeleo na kuwajengea uwezo vijana katika tafakari ya kujitambua wapi tumetoka, tuko wapi, tunakwenda wapi na wapi tujisahihishe kama taifa. Aidha Naibu Meya wa Manispaa ya Singida ambaye pia ni Diwani wa kata ya Mungumaji Mhe. Hassan Mkata ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Manispaa ya Singida. Mhe. Mkata ameendelea kusisitiza vijana kuwa wazalendo na waadilifu katika kulitumikia taifa la Tanzania na hasa wakimtanguliza Mwenyezi Mungu.
Hata hivyo Maadhimisho ya Sherehe za miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Wilaya ya Singida yameambatana na zoezi la uchangiaji damu kwa hiari kuokoa maisha.
Ilongero
Anuani ya Posta: Box 27, Singida
Simu: +25526502252
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.