• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

MHE. GONDWE AFANYA ZIARA YA KIKAZI KATA YA MUGHUNGA

Posted on: September 18th, 2024

Mkuu wa wilaya ya Singida Mhe. Godwin Gondwe akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya pamoja na baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida wamefanya ziara ya kikazi katika kata ya Mghunga leo tarehe 18/9/2024 kwa lengo la kukutana na wananchi na kusikiliza changamoto zao.

Akikaribisha ugeni huo mbele ya wananchi wa Kijiji cha Nduamghanga, diwani wa kata ya Mghunga, Mhe. Hassan Mtinangi aliipongeza serikali kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo afya, elimu na umeme. Pia alizungumzia mgogoro uliopo katika kata hiyo ukihusisha mpaka kati ya Kijiji cha Nduamghanga kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida na Kijiji cha Wairu kilichopo katika wilaya ya Chemba mkoa wa Dodoma, ambapo changamoto hiyo imekuwa ikiathiri shughuli za upigaji kura kila mara msimu wa uchaguzi unapofika.

“Huo mpaka tunaogombania, wenzetu wale wanatuhadaa bure, kutoka Wairu wanasema kwamba hapa ni kwao lakini lahasha hapa si kwao, sasa wao wanahadaiwa na watu baadhi na wapo ndani ya eneo letu,sasa kama tutakuwa huyu hapa wa Chemba huyu hapa wa Singida, hapa tutafanyaje kazi ya utendaji?” Alizungumza Mheshimiwa Mtinangi.

Vilevile Mkuu wa wilaya ya Singida alipata nafasi ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea maelekezo ambapo changamoto kubwa imeoneka kuwa ni mipaka baina ya vijiji na mipaka baina ya maeneo ya wananchi na hifadhi na misitu. Mhe. Gondwe alipata nafasi ya kutoa maelekezo juu ya namna ya utatuzi na kutoa wito juu ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

 “Mimi na wenzangu tumeona kwa macho, hivyo tukubaliane kuwa tumelipokea kwa namna ya pekee na tukaone utaratibu mzuri wa kulifanyia kazi ili usiathiri upigaji wa kura katika kitongoji cha Ukombozi. Naomba msijichukulie sheria mkononi mkagombana na wenzetu wa jirani,wale ni jirani zetu. Pia, tujiandikishe kwenye orodha ya kupiga kura, kuanzia tarehe 25 mwezi huu itaenda mpaka tarehe 1 Oktoba, naomba mjiandikishe, mjitokeze na mkijiandikisha msikose kupiga kura tarehe 27 Novemba mwaka huu. Kuhusu suala la msitu, maelekezo ni kama ifuatavyo; kwanza, mpango wakuendelea kutengeneza mipaka ile kama mlivyopanga washirikisheni wananchi wa eneo hili kupitia kwa viongozi, ili kuondoa hizi changamoto.…..Pili, tunapoendelea kutatua changamoto hii nawaomba tuvumiliane, tuache uchochezi maana huo sio utanzania, nchi yetu ni ya amani na mimi nawahakikishia usalama katika wilaya yetu ya Singida.”



Matangazo

  • TANGAZO LA BVR May 11, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA April 17, 2025
  • MAENEO YA UWEKEZAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA January 03, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI ZA MUDA July 17, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA SINGIDA WAPATA MAFUNZO KUHUSU USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KATIKA UWEKEZAJI

    April 03, 2025
  • TAWA YATOA ELIMU YA MBINU ZA KUKABILIANA NA WANYAMA PORI

    April 03, 2025
  • HALMASHAURI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI WATEMBELEA HALMASHAURI YA SINGIDA

    March 28, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AWAASA WALIMU KUEPUKA MIKOPO UMINZA

    March 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Mgogoro wa Ardhi Tarafa ya Mgori wamaliizika
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.