• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

MHE. HALIMA DENDEGO AWATAKA MADIWANI KUSIMAMIA UKUSANYAJI WA MAPATO YA NDANI.

Posted on: January 15th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, amewataka madiwani wa Manispaa ya Singida na Halmashauri ya Wilaya ya Singida (DC) kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa asilimia 100 pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato, ili kuimarisha ujenzi na ukarabati wa barabara pamoja na miundombinu mingine muhimu ya kijamii.


Mhe. Dendego ametoa wito huo leo Januari 15, 2026, wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa Waheshimiwa Madiwani yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa, yakilenga kuwajengea uwezo viongozi hao katika utekelezaji wa majukumu yao. Akizungumza katika hafla ya ufungaji mafunzo hayo, Mhe. Dendego amesema madiwani wana wajibu mkubwa wa kusimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato ya halmashauri zao, akisisitiza kuwa mapato hayo ndiyo nguzo ya maendeleo katika sekta mbalimbali. “Ukusanyaji wa mapato unatakiwa uwe wa asilimia 100. Ninyi madiwani ndiyo mnatakiwa kusimamia upatikanaji wa mapato haya, kwa kuwa ndiyo yanayosaidia ujenzi wa barabara, madarasa na miundombinu mingine muhimu. Haitakiwi kuwaambia wananchi wasilipe kodi; kodi hizi ni kwa maendeleo yao na ya nchi kwa ujumla,” amesema.


Kwa upande mwingine, Mhe. Dendego amewataka madiwani kuhakikisha usajili wa wanafunzi unafanyika kwa asilimia 100 katika kata zao, hususan kwa watoto wenye sifa za kuanza shule, na kusimamia kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa wanaripoti shuleni kwa wakati. Aidha, amewakumbusha madiwani kuendelea kusikiliza na kushughulikia kero za wananchi, akisisitiza kuwa jukumu lao la msingi ni kuwahudumia wananchi na kusimamia maendeleo katika maeneo yao. Mafunzo hayo ya siku tatu yalilenga kuwajengea uwezo madiwani katika masuala ya uongozi, usimamizi wa mapato, na uwajibikaji kwa jamii wanazoziongoza.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI January 20, 2026
  • TANGAZO LA MAUZO YA MAZAO YA MISITU December 05, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI November 20, 2025
  • TANGAZO LA BIMA December 05, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA YAFANYA TATHMINI YA MAOMBI YA MIKOPO YA ASILIMIA 10, KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU.

    January 27, 2026
  • KIHONGOSI AKAGUA MIRADI YA AFYA WILAYA YA SINGIDA

    January 19, 2026
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA YAIMARISHA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MAENDELEO

    January 17, 2026
  • KIKAO CHA KAMATI YA LISHE KWA ROBO YA PILI YA MWAKA

    January 16, 2026
  • Angalia zote

Video

VIJANA WANUFAIKA NA MIKOPO YA ASILIMIA 10
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.