Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida ndugu. Ally Mwendo akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Mhandisi Paskas Muragili kwenye zoezi linaloendelea la upandaji miti katika maeneo ya Shule ya Msingi Sekoutoure na Shule ya Sekondari inayoendelea kujengwa kijijini hapo. Jumla ya miti 100 ya kivuli na miti ya matunda imepandwa kijijini. Akizungumza na wananchi, walimu, wanafunzi na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Singida Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Singida ndugu Ally Mwendo amewaasa kwamba miti inayoendelea kupandwa kijijini hapo na maeneo mengine yote ya Wilaya ya Singida itunzwe ili kukabiliana na janga la ukame. Hata hivyo Ndugu. Issa Mwiru Mhe. Diwani wa Kata ya Ilongero ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika kata ya Ilongero Wilaya ya Singida na kutoa kipaumbele cha shughuli za huduma za Kijamii zinazoendelea wilayani humo kama kutembelea na kuhudumia watoto wenye ulemavu wanaoishi katika kituo cha kulelea watoto kiitwacho Ilongero Parish, shughuli za usafi wa mazingira, upandaji miti , huduma za kijamii zilizotolewa katika kituo cha afya Ilongero na Hospitali ya St. Carolus Mtinko pamoja na midahalo inayoendelea shule ya Sekondari Ilongero katika msimu wa Wiki ya Uhuru. Haya yote yamejiri kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Ilongero
Anuani ya Posta: Box 27, Singida
Simu: +25526502252
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.