• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Singida District Council
Singida District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI
    • Vitengo
      • TEHAMA na TAKWIMU
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • Michezo , Utamaduni na Sanaa
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, uongozi na mipango
      • Uchumi, ujenzi na mazingira
      • Huduma za jamii
      • VVU UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya madiwani
      • Kumuona mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA NEST

Posted on: January 21st, 2025

Mafunzo ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST),yametolewa kwa watumishi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida wakiwemo, Waalimu wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari,Waganga Wafawidhi wa Hospitali, Zahanati na Vituo vya Afya pamoja na Maafisa Watendaji Kata kuanzia siku ya jana tarehe 20/1/2025,lengo ikiwa ni kuongeza ufanisi na uaminifu katika kufanya manunuzi Serikalini.

Mafunzo hayo ya siku mbili,yametolewa na wawezeshaji kutoka Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma (PPRA) Kanda ya kati na Magharibi,ambapo watumishi hao wamepata nafasi ya kufundishwa namna ya kutumia mfumo huo wa manunuzi  na kuelezea changamoto wanazo kumbana nazo pindi watumiapo mfumo huo,na kupatiwa majibu juu ya changamoto hizo.

Akifunga mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Bi Janeth Mbugha,amewashukuru Wawezeshaji na kuwapongeza Watumishi wote waliohudhuria mafunzo,na kuwasisitizia watumishi hao kwenda kuwashirikisha watumishi walio chini yao, kile walichojifunza, ili kila mmoja awe na ujuzi wa kutumia mfumo huu pindi wanapohitaji kufanya manunuzi katika Idara au Vituo vyao vya kazi.

“Ukirudi peleka Mrejesho.Na itakuwa jambo jema zaidi kama mtaitana kama menejimenti,mkashirikishana haya yaliyopo.Kama leo niko hapa, kesho huwezi jua, mimi sina garantii ya maisha yangu,lakini kama nimewaelekeza wenzangu, kazi inaendelea.” Alisema Bi Janeth.

Mafunzo haya yamemalizika rasmi leo ikiwa ni siku ya pili,ambapo wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na baadhi ya wasaidizi kutoka katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri, nao wamepatiwa mafunzo hayo.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUKODISHWA KWA SHAMBA LA MBEGU LA MPAMBAA September 16, 2025
  • TANGAZO LA WATUMISHI KUHUSU WCF September 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI August 30, 2025
  • TANGAZO LA FURSA ZA KUTOA HUDUMA ZA CHAKULA (CATERING) KATIKA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA September 01, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MKUTANO MAALUM WA MAANDALIZI YA MSIMU WA KILIMO, WILAYA YA SINGIDA.

    October 03, 2025
  • TIMU YA UKAGUZI KUTOKA KIKOSI CHA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, YAFANYA UKAGUZI.

    October 02, 2025
  • MHE. GONDWE ATEMBELEA MIRADI YA LISHE KATIKA SHULE 3 ZA SEKONDARI.

    September 29, 2025
  • USAFI WA MAZINGIRA WAFANYIKA, KATA YA MUGHAMO

    September 26, 2025
  • Angalia zote

Video

WATUMISHI WAPYA WAASWA KUWEKA AKIBA
More Videos

Kurasa za karibu

  • Matangazo
  • Habari
  • Matukio

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti kuu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - Utumishi
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Jengo la Utawala Kijiji cha Mwahango Kata ya Ilongero

    Anuani ya Posta: Box 27, Singida

    Simu: +25526502252

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.