KUITWA KAZINI KWA WALIOFAULU USAILI WA NAFASI YA MTUNZA KUMBUKUMBU MSAIDIZI DARAJA II.pdf
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida anawaarifu waombaji waliofanya Usaili tajwa hapo juu na kufaulu kwa nafasi ya Mtunza Kumbukumbu Msaidizi Daraja II, kuwa wanatakiwa kuripoti kazini kuanzia tarehe 24 Novemba, 2022 mpaka tarehe 05 Disemba, 2022 katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Aidha, kila msailiwa ALIYEFAULU na KUITWA KAZINI anatakiwa kufika na Vyeti halisi vya Elimu na Taaluma (ORIGINAL CERTIFICATES), Picha mbili (Passport Size), Cheti cha Kuzaliwa pamoja na Kitambulisho cha Taifa au Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
Karibuni sana.
Ilongero
Anuani ya Posta: Box 27, Singida
Simu: +25526502252
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded.singidadc@singida.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Haki zote zimehifadhiwa.